Theolojia Katika Picha

4 9 6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Usomaji kuhusu Taipolojia (muendelezo)

kuhusiana na mada zinazohitaji kuangaziwa kitheolojia, kwa usahihi na ulinganifu wa kutuwezesha sisi, kwa kutumia chanzo hiki pekee, kufikia uelewa sahihi na kamili. Neno kivuli au mfano ( typos ) linahusika katika hili: • Linatokea mara moja, angalau, kwa maana ya kawaida ya alama au chapa inayotengenezwa au inayoachwa na kitu kigumu kwenye kitu kilaini (Yoh. 20:25 NEN) • Kwa kawaida hubeba maana ya jumla ya kielelezo , kiolezo , au mfano , lakini kwa upana mkubwa wa matumizi hadi kujumuisha kitu cha kuabudiwa, au sanamu (Mdo 7:43) • Kielelezo cha nje (kinachoonekana) kilichojengwa kwa ajili ya huduma ya Mungu (Mdo. 7:44; Ebr. 8:5) • Muundo au nakala ya waraka (Mdo 23:25) • Njia ya ufundishaji wa doktrini (fundisho la Biblia) iliyotolewa na wahubiri wa kwanza na waalimu wa Injili (Rum. 7:17) • Mhusika (kama katika riwaya, tamthilia, n.k) au, katika mitkadha fulani, mfano wa kawaida (Rum. 5:14; 1 Kor. 10:11; Flp. 3:17; 1 The.1:7; 1 Pet. 5:3). Hayo katika Maandiko ya Agano Jipya ni matumizi ya namna mbali mbali ya neno kivuli au mfano (yaliyojificha, hata hivyo, katika maneno mengine tofauti tofauti katika toleo lililoidhinishwa). Tunastaajabia kwa mshangao wa pekee uwezo na wepesi ambao baadhi ya ndugu wenye nia njema wanaonyesha katika kuona kile ambacho hakipo; vile vile tunapigwa na butwaa, tukighubikwa na uzito wa mioyo, kwa sababu ya ukiroho uliopindukia ambao wanaudhihirisha kwa kuyalazimisha maelezo ya wazi sana ya Maandiko yasiyo na chembe ya utata kuwa yenye maana adimu sana ya kiroho. “Vikapu vitatu vyeupe” ambavyo mwokaji wa Farao aliota vikiwa juu ya kichwa chake, kwetu sisi ni sehemu ya hadithi ya kweli iliyotokea; lakini kuona katika vikapu hivyo hivyo vitatu uhusiano wowote uliojificha na wa kina na fundisho la Utatu hufanya sehemu moja ya akili zetu kucheka na sehemu nyingine kuugua. Tunapata hisia kama hizo tunapohakikishiwa kwamba nywele za bibi harusi katika Wimbo Ulio Bora ni umati wa mataifa yaliyogeuzwa kuwa Wakristo. Uwezekano wa Matumizi Mabaya Mno ya Taipolojia ni Mkubwa

 J. Sidlow Baxter, The Strategic Grasp of the Bible .

Made with FlippingBook Digital Publishing Software