Theolojia Katika Picha
/ 4 9 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Usomaji kuhusu Taipolojia (muendelezo)
Ni jambo la kushitua fahamu kusikia kwamba “senti mbili” ambazo Msamaria Mwema alimpa mwenye nyumba ya wageni zilikuwa na maana fiche ya Ubatizo na Meza ya Bwana. Tunawahurumia sana kina Mathayo, Marko, Luka na Yohana, wakati mtumishi mwingine mhasiriwa wa ugonjwa wa taipolojia uchwara anapotuambia “mapipa manne” ya maji ambayo Eliya aliamuru yamwagwe juu ya madhabahu kwenye Mlima Karmeli walikuwa waandishi wanne wa Injili. Kuhusu kasisi ambaye angetushawishi kuamini kwamba mashua ambayo Bwana wetu alitumia kuvuka Galilaya ni Kanisa la Anglikana, wakati “meli nyingine ndogo” zilizoandamana nayo zilikuwa ni madhehebu mengine, hatuwezi kuepuka wazo la utukutu kwamba mfafanuzi wa riwaya mwenyewe, kama ile mashua, lazima pia alikuwa “baharini.” Tunahisi vivyo hivyo kuhusu maelezo ya Papa Gregory Mkuu kwa habari ya Ayubu, ambapo anadai kitenzi cha Ayubu “marafiki” kinawakilisha wazushi; na wanawe saba wanawakilisha Mitume kumi na wawili; kondoo wake elfu saba ni kivuli cha watu waaminifu wa Mungu na ngamia wake elfu tatu wenye vibyongo ni Wamataifa waliopotoka!”
Makosa Matatu ya Taipolojia ya Kuepukwa
Kuna hatari tatu, hata hivyo, ambazo lazima ziepukwe: • Kuwekea mipaka kivuli , na hivyo kutokitumia • Kukuza sana kivuli , na hiyo kukitumia kupita kiasi • Kubuni kivuli dhahania, na hivyo kukitumia vibaya
J. Boyd Nicholson kutoka utangulizi wa Harvest Festivals .
Hoja Dhidi ya “Mtazamo wa Kale” wa Taipolojia
Hoja dhidi ya taipolojia: • Inatafuta tu kupata “vivuli” vya Kristo kila mahali katika Agano la Kale. • Mungu aliweka matukio, taasisi, na/au watu katika Agano la Kale kwa kusudi kuu la kufanyika vivuli vya Kristo. Matokeo mawili mabaya ya hemenetiki hii ya zamani: • Hakuna haja sana ya kupata ukweli na maana katika matukio na watu wenyewe (kana kwamba Agano la Kale linakuwa mkusanyo wa vivuli).
Christopher J. H. Wright, Knowing Jesus through the Old Testament . Downers Grove: InterVarsity Press, 1992. uk. 115-116
Made with FlippingBook Digital Publishing Software