Theolojia Katika Picha

4 9 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Usomaji kuhusu Taipolojia (muendelezo)

• Kufasiri kila maelezo yasiyoeleweka ya “vivuli” vya Agano la Kale kama vielelezo vya Yesu (hemenetiki inageuka mazingaombwe, kama kumvuta sungura kutoka kwenye kofia). Hitimisho: taipolojia yenyewe peke yake sio njia ya kufasiri Agano la Kale. “Lakini tunaporudi nyuma na kusoma Zaburi ya 2 yote, Isaya 42 na Mwanzo 22, ni kweli vile vile kwamba zina ukweli na maana nyingi sana tunazohitajika kuchunguza ambazo hazihusiani moja kwa moja na Yesu mwenyewe. Taipolojia ni njia ya kutusaidia kumwelewa Yesu katika mwanga wa Agano la Kale. Sio njia pekee ya kuelewa maana kamili ya Agano la Kale lenyewe” (Wright, 116). Kukanusha Madai ya Wright • Yesu alitumia taipolojia (k.m., nyoka wa shaba, mana jangwani, Hekalu ambalo ni mwili wake, Mchungaji Mwema, n.k). • Mitume na wafasiri Wakristo wa kale walitumia taipolojia kama njia yao ya kawaida ya kusoma Agano la Kale (k.m., Musa kuupiga Mwamba, safari ya taifa la Israeli jangwani, Yesu kama Israeli wa pili, n.k). • Biblia inajirejea yenyewe kwa njia hii (k.m., Kitabu cha Waebrania, Hema, ukuhani, n.k). Swali: Je, tunapaswa kutumia Agano la Kale kama Yesu na Mitume walivyolitumia, kwa kurejelea taipolojia kwa kiasi fulani? Kristo anabeba ndani yake ukamilifu wa kanuni za Agano la Kale , kiini cha vivuli na mifano ya Agano la Kale , na utimilifu wa unabii wa Agano la Kale . Kweli zile kumhusu yeye zinazochipuka katika Agano la Kale zinachanua kikamilifu katika Agano Jipya; kienge cha ukweli wa kinabii kinageuka kuwa nuru kuu ya ufunuo wa kiungu. Vivuli vya Agano la Kale vimepata utimilifu wake katika Agano Jipya kwa njia kadhaa: (1) Maagizo ya maadili ya Agano la Kale yanatimizwa au kukamilishwa katika maisha na mafundisho ya Kristo. (2) kweli au kanuni za kitamaduni na za kawaida zilikuwa tu vivuli vya kiini cha kweli kinachopatikana katika Kristo. (3) Unabii wa Kimasihi uliotabiriwa katika Agano la Kale hatimaye ulitimizwa katika historia ya Agano Jipya. Katika kila moja ya mahusiano haya ni dhahiri kwamba maagano haya mawili yameunganishwa Hemenetiki ya Kikristolijia: Masihi Yesu Anaunganisha AK na AJ

 Norman Geisler, To Understand the Bible Look for Jesus . (1979) 2002. uk. 68

Made with FlippingBook Digital Publishing Software