Theolojia Katika Picha

/ 4 9 9

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Usomaji kuhusu Taipolojia (muendelezo)

kwa namna ambayo hayawezi kutenganishwa. Hili Jipya sio tu nyongeza kwa lile la Kale bali ni kikamilisho chake muhimu. Kama vile kitabu cha Waebrania kinavyosema, “Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao [waamini wa Agano la Kale] wasikamilishwe pasipo sisi” (Ebr. 11:40). Kwa maana yale yaliyomo katika Agano la Kale yamefafanuliwa kikamilifu katika Agano Jipya tu.

Jinsi Paulo na Mitume Walivyosoma Maandiko

Kama inavyoweza kuonekana wazi, utaratibu wa kihemenetiki ambao Paulo na waandishi wengine wa Agano Jipya wanautumia kufasiri Sheria katika maana ya kiroho ni wa mafumbo, kwa maana kwamba wanafunua maana nyingine zaidi ya maana ya msingi au ya moja kwa moja kutokana na kifungu kilichotolewa. Neno la kawaida ambalo Paulo anatumia ili kufafanua uhusiano kati ya viwango viwili vya maana ni typos = umbo, mfano, ishara, au kivuli (Rum. 5:14; 1 Kor. 10:6, nk.); lakini katika Wagalatia 4:24, ambapo anawaonyesha wana wa Hajiri na Sara kuwa vifananisho vya Wayahudi na Wakristo, anasema ‘Mambo haya husemwa kwa mfano ( allegorouumena )’, akionyesha kwamba aliona neno ‘ typos ’ kuwa ni sawa na ‘mfano.’ Kwa kuheshimu istilahi za Paulo, wasomi wa kisasa wanaita aina hii ya tafsiri – ambayo, kama tutakavyoona, ilipata mafanikio makubwa na ikawa njia halisi ya Kikristo ya kusoma Agano la Kale – ‘taipolojia’ au ‘ufasiri wa kitaipolojia.’ Hapo zamani [yaani. katika nyakati za kale] iliitwa ya ‘kiroho’ au ya ‘kifumbo.’ Ilitokana na imani thabiti kwamba Sheria ya zamani ilielekezwa kimkakati kwenye tukio kuu la Kristo, na kwamba, kwa sababu hiyo, ambao wangeweza kutoa maana yake halisi na kamilifu ni wale tu walioifasiri katika muktadha wa Kristolojia.

 Manlo Simonetti, Biblical Interpretation in the Early Church . uk. 11-12

Made with FlippingBook Digital Publishing Software