Theolojia Katika Picha

5 0 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Usomaji kuhusu Unabii wa Kimasihi Mch. Dkt. Don L. Davis

Rudolph Bultmann na Utabiri wa Mateso na Ufufuo

Na Yesu angefikiriaje uhusiano wa kurudi kwake kama Mwana wa Adamu na kazi yake ya sasa ya kihistoria ? Angelazimika kutegemea kuondolewa duniani na kuinuliwa hadi mbinguni kabla ya ule Mwisho, yaani, ujio wa Utawala wa Mungu, ili aje kutoka huko juu ya mawingu ya mbinguni kushika wadhifa wake halisi. Lakini angefikiriaje kuondolewa kwake duniani? Kama kuhamishwa kimuujiza? Miongoni mwa maneno yake hakuna dokezo la wazo lolote la ajabu kama hilo. Kama kuondoka kwa njia ya kifo cha asili, basi? Kuhusu hilo, pia, maneno yake hayasemi chochote. Kwa kifo kikatili, basi ? Lakini ikiwa ni hivyo, je, angeweza kutegemea hilo kuwa jambo la uhakika kabisa—kama ambavyo ufahamu wake kuhusu kuinuliwa kwenye adhama ya Mwana wa Adamu ajaye ulikuwa wa uhakika? Kwa hakika, tabiri za mateso (Mk. 8:31; 9:31; 10:33-34; rej. 10:45; 14:21, 41) zinatangulia kueleza kuuawa kwake kama ilivyoamriwa na Mungu tokea awali. Lakini je, kunaweza kuwa na shaka kwamba zote ni vaticinia ex eventu? Mbali na hilo, hazisemi juu ya parousia yake! Na tabiri za parousia (Mk 8:38; 13:26-27; 14:62; Mt. 24:27, 37, 44) kwa upande wake, hazizungumzi juu ya kifo na ufufuo wa Mwana wa Adamu. Kilicho dhahiri ni kwamba utabiri wa parousia hapo awali haukuwa na uhusiano wowote na utabiri wa kifo na ufufuo; yaani, katika semi zinazozungumza juu ya kuja kwa Mwana wa Adamu hakuna wazo kwamba Mwana wa Adamu tayari yuko hapa katika mwili na lazima aondolewe na kifo kabla ya kurudi kutoka mbinguni. Ufasiri wa Kibiblia wa Kisasa: Si Kilichotokea , lakini Kanisa Lilihubiri Nini? Sasa ni kweli kwamba katika utabiri wa mateso dhana ya Kiyahudi ya Masihi-Mwana wa-Adamu inafasiriwa upya – au kwa ubora zaidi, inatajirishwa kwa kukusanywa pamoja – kwa vile ambavyo wazo la kuteseka, kufa, kufufuka kwa Masihi au Mwana wa Adamu halikujulikana katika dini ya Kiyahudi. Lakini tafsiri hii mpya ya dhana hii haikufanywa na Yesu mwenyewe bali na Kanisa ex eventu [baadaye, yaani baada ya kuwa na taarifa zote] . Bila shaka, kuna jaribio linalofanywa ili kubeba wazo la Mwana wa Adamu anayeteseka kurudi katika mtazamo wa Yesu mwenyewe kwa kudhani kwamba Yesu alijiona kama

 Rudolph Bultmann, Theology of the New Testament. Vol. 1. Trans. Kendrick Grobel. New York: Charles Scribner’s Sons, 1951. uk. 29-30

 Rudolph Bultmann, Theology of the New Testament. Vol. 1. uk. 31

Made with FlippingBook Digital Publishing Software