Theolojia Katika Picha

/ 5 0 1

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Usomaji kuhusu Unabii wa Kimasihi (muendelezo)

Deutero – Mtumishi wa Mungu wa unabii wa Isaya ambaye anateseka na kufa kwa ajili ya wenye dhambi, na kuunganisha pamoja mawazo hayo mawili. Mwana wa Adamu na Mtumishi wa Mungu katika sura moja ya Mwana wa Adamu anayeteseka, anayekufa na kufufuka. Awali ya yote, mashaka ambayo lazima yatolewe kuhusu historia ya utabiri wa mateso ni yale yanayozungumza dhidi ya jaribio hili. Kwa kuongezea, mapokeo ya maneno ya Yesu hayaonyeshi dalili zozote kwamba alijitambua mwenyewe kama Mtumishi wa Mungu wa Isaya 53 . [Kwa Kanisa la kwanza] lilikuwa jambo la maana kubwa zaidi na la kuvutia zaidi kwamba Bwana aliyefufuka alikuwa yeye ambaye hapo awali alikufa msalabani. Hapa pia, semi zinazofanana na dhana hiyo zinajitokeza upesi, kama vile mapokeo ya 1 Wakorintho 15:3-4 yanavyoonyesha tena, na pia maelezo kwenye Warumi 4:25: “ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.”— Kauli ambayo ni dhahiri kwamba ilikuwepo kabla ya Paulo na alikuwa ameipokea.... Jambo hili hili linaonyeshwa na utabiri uliowekwa katika kinywa cha Yesu katika Marko (na pia katika Mathayo na Luka) ukirudisha kerygma ya Kiyunani katika mahubiri ya Yesu. 2 Petro 1:19-21 - bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. Maswali kuhusu unabii wa Masihi 1. Unabii unasema nini hasa? 2. Ni kwa jinsi gani maisha na huduma ya Yesu vinaakisi kwa uwazi ujumbe huo wa unabii ? 3. Unaangazia vipi ufahamu wangu wa… Mpango mkuu wa Mungu wa kusimamisha tena utawala wa ufalme wake? Mipango ya adui ya kuudhoofisha? Kile tunachoweza kutazamia Mungu anapolitimiza Neno lake? Unabii wa Kimasihi: Kitu cha Hakika Zaidi

 Rudolph Bultmann, Theology of the New Testament. Vol. 1. uk. 82-83

Made with FlippingBook Digital Publishing Software