Theolojia Katika Picha
5 0 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Usomaji kuhusu Utumishi
Mtazamo wa Yesu kuhusu Utumishi
Yesu anapozungumza na wanafunzi wake kuhusu utumishi, ana mambo mawili akilini. Kwanza ni utumishi unaotolewa kwa Mungu kama mamlaka kuu ambayo kwayo wanawiwa utii wao, na pili ni huduma wanayotoa kwa watu kama tendo la unyenyekevu na upendo . ~ David Bennett. Metaphors of Ministry. uk. 25
Kufuata Nyayo za Bwana Mwenyewe: Yesu kama Mtumishi
Ni katika suala kama [utumishi] ambapo ninaona sifa moja inayowatofautisha Wakristo na ulimwengu: tunatumika kwa sababu Kristo alikuwa mtumishi na alituelekeza waziwazi tufanye hivyo kwa kumbukumbu yake. Hatupaswi kutumika kwa sababu inatufanya tujisikie vizuri au inafanyika kama aina fulani ya matibabu. Hatupaswi kutumikia kwa sababu ni mfano mzuri kwa watoto wetu. Hatupaswi kutumikia kwa sababu itafanya mambo katika jamii yaende vizuri na kwa wepesi zaidi. Tunatumika kwa sababu Kristo alikuwa mtumishi. ~ Kenneth H. Carter, Jr. The Gifted Pastor. uk. 495
Made with FlippingBook Digital Publishing Software