Theolojia Katika Picha
5 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Huduma ya Kusifu na Kuabudu Mch. Dkt. Don L. Davis
Wito Maalum katika Huduma ya Kusifu na Kuabudu
Sifa iletayo ushindi si sifa ya hapa na pale tu au ya kimatukio, sifa ambayo hubadilika-badilika kulingana na hali na mazingira. Ni sifa endelevu, sifa ambayo ni wito, mfumo wa maisha. “Nitamhimidi Bwana kila wakati; sifa zake zi kinywani mwangu daima” (Zaburi 34:1). “Heri wakaao nyumbani mwako; wanakuhimidi daima” (Zaburi 84:4). Imeelezwa kwamba huko mbinguni sifa ni muhimu sana kiasi kwamba ndio jukumu kuu la tabaka fulani la viumbe (Ufunuo 4:8). Mungu alimpa Mfalme Daudi ufunuo wa umuhimu na nguvu ya sifa duniani kiasi kwamba, kwa kufuata utaratibu wa mbinguni, alitenga na kuweka wakfu jeshi la Walawi elfu nne ambao kazi yao pekee ilikuwa ni kumsifu Bwana! (1 Nyakati 23:5). Hawakufanya kitu kingine chochote. Mojawapo ya matendo rasmi ya mwisho ya Mfalme Daudi kabla ya kifo chake lilikuwa kuweka mpangilio na muundo rasmi wa sifa. Kila asubuhi na kila jioni kikosi cha Walawi hao elfu nne kilihusika katika utumishi huu, “nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana, na jioni vivyo hivyo” (1 Nyakati 23:30). Kwa aibu na kushindwa kwa Kanisa, umuhimu wa sifa ambao umejaa katika maudhui ya Neno umepuuzwa kwa kiasi kikubwa. Ili kuwa na matokeo zaidi, basi, sifa lazima ziwe kubwa, endelevu, tabia isiyobadilika, shughuli ya wakati wote, wito unaofuatiliwa kwa bidii, mfumo kamili ya maisha. Kanuni hii inasisitizwa katika Zaburi 57:7 : “Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.” Hii inamaanisha tabia iliyopangwa na iliyoamuliwa mapema ya kusifu. «moyo wangu NI THABITI.» Aina hii ya sifa inategemea kitu fulani zaidi ya furaha ya muda. ~ Paul Billheimer, Destined for the Throne , uk. 121-22. I. Kusudi lililoinuliwa na lenye kumwelekea Mungu, Zab. 150:5; Ufu. 4:11; Zab. 29:1-2 A. “Ndiyo maana tunamsifu, ndiyo sababu tunaimba!” 1. Kuonyesha furaha yetu katika Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu 2. Kukiri neema ya Mungu katika Yesu Kristo 3. Kupata uzoefu wa uwepo wa Mungu 4. Kuona uzuri wa Mungu katikati ya watu wake
Made with FlippingBook Digital Publishing Software