Theolojia Katika Picha

5 2 6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Wasifu wa Mwanafunzi wa Karne ya 21 (muendelezo)

4. Anadumisha uaminifu katika ushirika ndani ya Mwili, kwa kushiriki kikamilifu katika kusanyiko la waaminio la mahali pamoja (Yohana 13:34-35). a. Amebatizwa katika imani kwa msingi wa ungamo lake la imani katika Yesu Kristo b. Anashiriki kikamilifu katika ibada ya pamoja na maadhimisho ya Mwili kupitia kusifu, kuabudu, na Meza ya Bwana. c. Anakusanyika mara kwa mara na washirika wengine wa Mwili ili kulijenga kanisa kupitia ushirika, maombi, huduma, na sherehe. d. Anatumia karama zake katika huduma kwa kutumika pamoja na washirika wengine wa Mwili. e. Anawasilianamara kwamara naMwili katika namna inayoujenga na kuuimarisha. a. Anaomba kwa uthabiti na kwa bidii kwamba Bwana ainue watenda kazi katika mavuno yake popote pale ambapo Kristo hajajulikana, kuabudiwa, na kutukuzwa. b. Anatoa kwa ukarimu wakati na rasilimali zake kuelekea uinjilisti na umisheni kama Mungu anavyomwongoza. c. Hutafuta fursa za kuwashirikisha wengine ushuhuda wake binafsi ili kuwavuta kwa Kristo. d. Anatumia muda kusimika waongofu wapya katika imani kwa kuwajumuisha katika Mwili. e. Humwomba Roho nafasi ya kuwafuasa wanafunzi wa kristo waaminifu ambao wanaweza kuwa watenda kazi pamoja naye katika kutimiza Agizo Kuu. 5. Anatekeleza mkakati thabiti wa kufanya wanafunzi wa Yesu ndani na nje ya nchi (Yoh. 20:21).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software