Theolojia Katika Picha

/ 5 2 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Wasifu wa Mwanafunzi wa Karne ya 21 Mch. Dkt. Don L. Davis

1. Anafurahia ushirika wa karibu na Bwana (Yohana 10:1-6; 15:12-14). a. Anapatikana bila masharti kwa Kristo kama Bwana (amejazwa na Roho Mtakatifu). b. Ana njaa ya kuwa zaidi na zaidi kama Kristo katika maono, tabia, na huduma. c. Maisha madhubuti ya ibada binafsi, kutafakari, na maombi. d. Mtindo wa maisha wa kusifu, kuabudu, na kusherehekea. e. Tumaini la kudumu katika uongozi na upaji wa Mungu katika Kristo. f. Anamtukuza Mungu katika hekalu la mwili wake, akili na roho yake. 2. Anashikilia msimamo wa imini uliojengwa juu ya maono ya kibiblia ya Kristo na Ufalme wake (Yohana 8:31-32). a. Uelewa wa kina wa Maandiko Matakatifu (yaani mada, historia, na kanuni zake kuu). b. Anadumisha mtazamo wa ulimwengu wenye msingi wa Kristo, kuona maisha katika mtazamo wa Mungu. c. Amejikita katika misingi ya imani, anaweza kuishirikisha kwa wengine na kuifafanua. d. Uwezo unaokua wa kutumia kwa halali Neno la kweli (yaani, kusikia, kusoma, kujifunza, kukariri, na kutafakari). e. Kuongeza uwezo wa kupigania imani dhidi ya upinzani wote. 3. Anaonyesha mwenendo wa kimungu katika mwenendo na mtindo wa maisha nyumbani, kazini na katika jamii (Yohana 17:14-23). a. Anaenenda kama inavyomstahili Bwana katika usemi, usafi, mwenendo, imani, na tabia. b. Anatimiza kwa kujidhabihu majukumu mbalimbali kama mshirika mchamungu katika nyumba yake na familia yake. c. Anamwakilisha Kristo kazini kwake katika ubora, moyo wa utumishi, heshima, na nia moja. d. Anadumisha sifa za kimungu katikati ya marafiki, majirani, na jamii.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software