Theolojia Katika Picha

5 2 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Washiriki wa Timu ya Paulo (muendelezo)

Onesimo , mzaliwa wa Kolosai na mtumwa wa Filemoni aliyemtumikia Paulo, Kol. 4:9; Flm. 10. Hermogene , mshiriki wa timu ambaye alimtelekeza Paulo gerezani, 2 Tim. 1:15. Figelo , mwenzake na Hermogene ambaye pia alimgeuka Paulo huko Asia, 2 Tim. 1:15. Prisila (Priska) , mke wa Akila wa Ponto na mtenda kazi mwenza katika Injili, Mdo 18:2, 18, 26; Rum. 16:3; 1 Kor. 16:19. Pude , Mroma, mwandamani wa Paulo, 2 Tim. 4:21. Sekundo , mwandamani wa Paulo alipokuwa njiani kutoka Uyunani kwenda Siria, Mdo 20:4. Sila , mfuasi, mtenda kazi mwenza, na mfungwa pamoja na Paulo, Mdo 15:22, 27, 32, 34, 40; 16:19, 25, 29; 17:4, 10, n.k. Sopatro , alifuatana na Paulo hadi Shamu, Mdo. 20:4. Sosipatro , jamaa ya Paulo, Rum. 16:21. Silvano , pengine jina la pili la Sila, 2 Kor. 1:19; 1 The.1:1; 2 The.1:1. Sosthene , Mtawala Mkuu wa sinagogi la Korintho, mtenda kazi pamoja na Paulo huko, Mdo 18:17. Stefana , mmoja wa waamini wa kwanza wa Akaya na mgeni wa Paulo, 1 Kor. 1:16; 16:15; 16:17. Sintike , mmoja wa wanawake “watenda kazi wenza” wa Paulo huko Filipi, Flp. 4:2. Tertio , mtumwa na mtu aliyeandika Waraka kwa Warumi, Rum. 16:22. Timotheo , kijana wa Listra wa mama Myahudi na baba Myunani ambaye alikuwa na bidii kubwa pamoja na Paulo katika huduma yake, Mdo 16:1; 17:14, 15; 18:5; 19:22; 20:4; Rum. 16:21; 1 Kor. 4:17; 16:10; 2 Kor. 1:1, 19; Fil. 1:1; 2:19; Kol. 1:1; 1 The.1:1; 3:2, 6; 2 The.1:1; 1 Tim. 1:2, 18; 6:20; 2 Tim. 1:2; Flm. 1; Ebr. 13:23. Tito , mfuasi Myunani na Mtenda kazi mwenza wa Paulo, 2 Kor. 2:13; 7:6, 13, 14; 8:6, 16, 23; 12:18; Gal. 2:1, 3; 2 Tim. 4:10; Tito 1:4. Trofimo , mfuasi wa Efeso aliyeambatana na Paulo kwenda Yerusalemu kutoka Uyunani, Mdo 20:4; 21:29; 2 Tim. 4:20. Trifena na Trifosa , wanafunzi wa kike wa Rumi, labda mapacha, ambao Paulo anawaita watenda kazi katika Bwana, Rum. 16:12. Tikiko , mfuasi wa Asia Ndogo aliyeambatana na Paulo katika safari mbalimbali, Mdo 20:4; Efe. 6:21; Kol. 4:7; 2 Tim. 4:12; Tito 3:12. Urbano , mfuasi wa Kirumi na msaidizi wa Paulo, Rum. 16:9.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software