Theolojia Katika Picha
5 3 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Wokovu Kama Kujiunga na Watu wa Mungu Terry Cornett
I. Njia muhimu zaidi ya kufafanua wokovu katika muktadha wa kibiblia ni kuuelezea kama kuunganishwa na watu wa Mungu. A. Agano la Kale 1. Mfano wa Agano la Kale wa wokovu ni Kutoka ambapo Mungu “aliwaokoa” watu wake kutoka utumwani huko Misri. a. Kuokolewa kulimaanisha kuunganishwa na watu waMungu waliokuwa wakitolewa pamoja kutoka utumwani na kuwekwa moja kwa moja chini ya ubwana, sheria, ulinzi, upaji na uwepo wa Mungu. b. Kutoka 6:7 – name nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. (rej. Law 26:12; Kumb. 4:20, Hos. 13:4). 2. Kuchaguliwa kwa Israeli na Mungu kuwa “watu wake” kuliwapa nafasi ya pekee kati ya watu wote wa dunia. a. Kumbukumbu 7:6 – Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi. b. Kumbukumbu 27:9 – Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa Bwana, Mungu wako. 3. Njia ya wokovu kwa yeyote aliye nje ya Israeli ilikuwa ni kujiunga na watu wa Mungu. a. Kutoka 12:37-38, 48 – Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. 38 Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana. 48 Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake
Made with FlippingBook Digital Publishing Software