Theolojia Katika Picha

/ 5 3 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Wokovu Kama Kujiunga na Watu wa Mungu (muendelezo)

wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle b. Isaya 56:3-8 – Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. 4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6 Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; 7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. 8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa. 4. Agano Jipya linadokeza kwamba hata Musa (wa asili ya Kiebrania lakini aliyelelewa kitamaduni kama Mmisri na kwa hivyo mgeni) alilazimika kufanya uamuzi wa kujumuika na watu wa Mungu kwa imani ili apate wokovu. Waebrania 11:24-25 – Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; 25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo 5. Muhtasari: [Katika Agano la Kale] wokovu ulikuja, si kwa sifa tu ya mwanadamu, bali kwa sababu mwanadamu alikuwa wa taifa lililochaguliwa kipekee na Mungu (“Salvation,” International Standard Bible Encyclopedia [Toleo la Kielektroniki]. Cedar Rapids: Parsons Technology, 1998.).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software