Theolojia Katika Picha

5 3 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Wokovu Kama Kujiunga na Watu wa Mungu (muendelezo)

B. Agano Jipya (Tito 2:14 – ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema) 1. Petro na Paulo wote wawili wanadokeza kwamba mtazamo wa Agano Jipya wa wokovu, kama ulivyokuwa katika Agano la Kale, unahusisha Mungu kuwaita watu, lakini watu “walioitwa” wanafungamanishwa na Kristo na Kanisa lake badala ya kufanyika “taifa” la kisiasa au kikabila. a. 1 Petro 2:9-10 – Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. b. Matendo 15:14 - Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. c. Waefeso 2:13, 19 - Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. 19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. d. Warumi 9:24-26 - ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? 25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. 26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai. 2. “Kwa upande mwingine, wakati ambapo ujumbe wa [Injili] unaohusika katika kila jambo ni chaguo la kimsimamo la mtu binafsi, lakini mtu aliyeukubali aliingia katika uhusiano wa kijamii na wale wengine waliotangulia kuchagua uhusiano huo. Kwa hiyo wokovu ulihusisha kuingizwa katika jumuiya ya utumishi (Marko 9:35, nk.)” ( International Standard Bible Encyclopedia [Toleo la Kielektroniki]).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software