Theolojia Katika Picha

/ 5 3 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Wokovu Kama Kujiunga na Watu wa Mungu (muendelezo)

II. Sitiari za Wokovu: Kuunganishwa kwa Watu.

Katika jamii ya wanadamu, kuwa mali ya “watu” (familia, ukoo, taifa) hutokea kupitia ama: • kuzaliwa, • kuasiliwa, au • kuolewa katika familia fulani Kwa hiyo, lugha ya wokovu katika Agano Jipya inatokana na sitiari hizi tatu za msingi katika kuelezea kile kinachotokea wakati wa wokovu. A. Kuzaliwa 1. Yohana 1:12-13 – Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. 2. Yohana 3:3 – Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 3. 1 Petro 1:23 – Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 4. 1 Petro 1:3 – Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu. B. Kuasiliwa 1. Warumi 8:23 – Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu. 2. Waefeso 1:4-6 – kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software