Theolojia Katika Picha

6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Baadhi ya Njia Ambazo Wakristo Hawakubaliani kuhusu Utakaso Mch. Terry G. Cornett

I. Maswali Mawili ya Msingi

A. Swali la kwanza: Je, mtu anaweza kutakaswa na kutengwa (kabisa kutoka kwenye dhambi), katika maisha haya ya sasa?

1. Makanisa ya Reformed /Kibaptisti na baadhi ya theolojia za Kipentekoste wanasema HAPANA.

2. Makanisa ya Holiness na baadhi ya theolojia za Kipentekoste wanasema NDIO.

B. Swali la Pili: Je, utakaso ni tukio la pili na la tofauti kutoka kwa Mungu, linalopokelewa kwa neema kwa njia ya imani? Unachoamini kuhusu swali la kwanza, kwa kawaida kinaathiri kile unachoamini kuhusu swali la pili.

1. Ikiwa unaamini kwamba utakatifu kamili hauwezi kutokea hadi siku ya kufa au kurudi kwa Kristo, maana yake una Imani ya kukua katika utakatifu lakini huamini kwamba kuna hatua tofauti katika maisha haya ambapo unaweza kufikiwa ukamilifu wa utakatifu.

2. Ikiwa unaamini kwamba utakatifu kamili unaweza kufikiwa, unajua lazima uje kupitia tukio au tendo la kubadilishwa (huwezi kuufikia kwa juhudu na bidii yako mwenyewe). Kwa hivyo wale wa Makanisa ya Holiness na Pentecostal-Holiness wanasema lazima kuna tukio la pili la kitofauti katika mchakato huu.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software