Theolojia Katika Picha

/ 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Baadhi ya Njia Ambazo Wakristo Hawakubaliani kuhusu Utakaso (muendelezo)

II. Mafundisho Kulingana na Mapokeo ya Reformed

A. Utakaso unaanza wakati wa wokovu na unaendelea hatua kwa hatua mpaka siku ya kutukuzwa. Mungu hututakasa kikamilifu kwa namna ya kututenga na kutuingiza moja kwa moja kwenye ufalme wake wakati wa wokovu, lakini utakaso wa sisi kuwa mbali na dhambi unafanywa kutokana na tunavyoenenda hatua kwa hatua na kila siku.

B. Dhambi kimsingi inafafanuliwa kama “kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”

C. Hoja zinazounga mkono:

1. Yesu alitufundisha wanafunzi wake kusali kila siku, “Utusamehe makosa yetu” (Mt. 6:12) na kuongeza “Lakini msipowasamehe wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” (Mt. 6:15).

2. Kanisa la Korintho lilitambulishwa na Paulo kama “lililotakaswa na Kristo Yesu na kuitwa kuwa takatifu” lakini kiuhalisia wa maisha yao hali ilikuwa tofauti kabisa. Paulo alisema katika 1 Wakorintho 3:3, “kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?” Paulo alielewa tofauti kati ya kutakaswa machoni pa Mungu lakini kuwa bado katika mchakato wa utakaso kimatendo.

a. Uzoefu unatufundisha kwamba: (1) Tunatenda dhambi.

(2) Watu wanaojidai kuwa wakamilifu huwa na tabia ya kushika sheria fulani, kulaani, kujisifu, na huwa na mwelekeo wa kukana dhambi inapotokea.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software