Theolojia Katika Picha

6 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Ili Tuwe Umoja Vipengele vya Harakati Jumuishi za Kupanda Makanisa Miongoni mwa Maskini wa Mjini Mch. Dkt. Don L. Davis Harakati za Kupanda Makanisa Miongoni mwa Maskini Mijini = maendeleo jumuishi na ya hima ya Ufalme wa Mungu katikati ya maskini wa mijini yenye matokeo ya ongezeko kubwa la makanisa ya kienyeji ambayo kimsingi yanafanana katika vipengele vingi vinavyoyapa utambulisho, kusudi, na utendaji wa tofauti na wa kipekee. Huduma miongoni mwa maskini wa mijini lazima iwe na msingi katika mtazamo na ufahamu wa uhuru tulionao katika Kristo ili kuwa na maono ya harakati jumuishi na zenye mafungamano za wafuasi wa Yesu ambao kwa sababu ya uzoefu wa pamoja, ukaribu, utamaduni, na historia yao wameamua kuakisi imani yao na ukristo wao kipekee kwa namna inayolingana na imani ya kihistoria lakini katika muktadha wa maisha yao na nyakati zao . Hiki si kitendo cha kiholela; harakati haziwezi kupuuza asili ya Kanisa moja (umoja), takatifu (utakatifu), katoliki (la ulimwengu wote), na la kitume (utume), watu wa pekee wa kweli wa Mungu. Hata hivyo, kama ilivyothibitishwa na viongozi wanaoibukia wa Kanisa la Kianglikana la Marekani (American Episcopal Church) wakati huo, uhuru tulio nao katika Kristo unaruhusu aina na matumizi tofauti ya ibada katika Mwili wa Kristo bila hatia yoyote, ilimradi tu tunatunza uaminifu wetu kwa mafundisho halisi ya kihistoria ya Kanisa kama yalivyofundishwa kwetu na manabii na mitume wa Bwana wetu. Fundisho lazima libaki kuwa kamili na lenye msingi imara; nidhamu, hata hivyo, zinaweza kutegemea mahitaji ya watu wanaozikumbatia, maadamu yote yanayowekwa na kufanyika yanaujenga Mwili wa Kristo, na kumtukuza Mungu Baba yetu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. “Makanisa Ambayo ni Sehemu ya Harakati Jumuishi za Upandaji Makanisa Miongoni mwa Maskini Mijini kwa Pamoja Yataakisi ”: 1. Historia moja na utambulisho mmoja (yaani, jina moja na urithi mmoja ). Harakati za Kupanda Makanisa miongoni mwa maskini wa mijini zitatafuta kujiungamanisha na kujitambulisha kwa msingi wa historia na utambulisho uliyofafanuliwa vyema ambao kwa furaha washirika wote na makusanyiko yao wanashiriki. 2. Liturujia na sherehe zinazofanana (yaani, ibada inayofanana ). Harakati za Kupanda Makanisa miongoni mwa maskini wa mijini zinapaswa kuakisi msingi mmoja wa utunzi na uimbaji wa nyimbo, uendeshaji wa sakramenti, mwelekeo na taswira ya kitheolojia, mtazamo kuhusu ujumi, mavazi, utaratibu wa kiliturujia, ishara, na malezi ya kiroho ambayo yanatuwezesha kumwabudu na kumtukuza

Ni sehemu ya thamani sana ya ule “uhuru uliobarikiwa ambao kwa huo Kristo alituweka huru,” ili katika ibada yake iweze kuruhusiwa miundo na matumizi mbali mbali bila hatia, ilimradi tu kiini cha Imani kitunzwe kikamilifu; na kwamba, katika kila Kanisa, kile ambacho hakiwezi kutambuliwa waziwazi kuwa cha Fundisho lazima kielekezwe kwenye Nidhamu; na kwa

hiyo, kwa ridhaa na mamlaka ya pamoja, kinaweza kubadilishwa,

kufupishwa, kupanuliwa,

kurekebishwa, au vinginevyo kuondolewa, kama itakavyoonekana inafaa zaidi kwa ajili ya kuwajenga watu, “kulingana na mahitaji mbalimbali ya nyakati na matukio.” ~ 1789 Dibaji ya Kitabu cha Maombi

ya Pamoja. 1928 Toleo la Kiaskofu.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software