Theolojia Katika Picha

/ 6 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Huduma ya Kusifu na Kuabudu (muendelezo)

3. Awamu ya tatu: yetu ni sahihi , yao ni ya kutiliwa shaka kiasi fulani 4. Awamu ya nne: yangu imeamriwa na Mungu na ni ya kiwango cha juu kuliko zote , ila za wengine wote si za kawaida na si sahihi.

D. Kuchanganya: uthibitisho wa umuhimu wa utofauti wa kujieleza na kushikilia mapokeo katika uzoefu wetu wa ibada katika Mungu. Je, unachanganyaje? 1. Katika nyimbo unazochagua 2. Katika mahadhi (aina) unazopiga 3. Katika ala unazochagua 4. Katika mipangilio ya sauti unayochagua. E. Kuheshimu utofauti huku ukiruhusu mapendeleo na upekee wa kujieleza: changamoto ya mara kwa mara ya kiongozi wa ibada 1. Unganisha huduma na uthamini wa kweli wa aina mbalimbali za muziki 2. Ongeza umaana kwa kupiga muziki uleule katika mahadhi tofauti. VIII. Mukhtasari wa Ibada: Kumtukuza Mungu Katika Mwafaka Unaompendeza Mungu A. Washirika wa nyumba ya Mungu: kuabudu kama kielelezo cha roho zilizookolewa B. Imejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Yesu Kristo kama Jiwe kuu la Pembeni na la Thamani: ibada kama mwitikio kwa ufunuo wa kihistoria wa Mungu kupitia Neno lake. C. Kuunganishwa pamoja kama hekalu takatifu katika Bwana: ibada kama hali ( atmosphere ) ya watu wa Mungu na kufanyika hekalu takatifu ambamo sifa zake zinakaa. D. Kujengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho: sisi wenyewe tu mahali ambapo sifa za Mungu zinaanzia na ambapo Mungu anakaa. E. Tunaweza kuunda mwafaka wa pamoja kwa kuleta pamoja vile tulivyo na yale tunayofanya kama viongozi, kusanyiko, na timu ya kuabudu katika dhabihu za sifa tamu na safi vya kutosha kwa ajili ya Mungu wetu kukaa!

Waefeso 2:19-22 – Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. 22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software