Theolojia Katika Picha

6 6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Ili Tuwe Umoja (muendelezo)

makusanyiko mapya haraka iwezekanavyo katika maeneo ya miji ambayo hayajafikiwa. 10. Maono ya pamoja ya miungano na ushirika (yaani, ushirikiano wa pamoja ). Harakati za Kupanda Makanisa miongoni mwa maskini wa mijini lazima zitafute kufanya miungano, makubaliano ya ushirika, na mahusiano mapya na makundi mengine kwa ajili ya mawasiliano ya mara kwa mara, ushirika, na umisheni. Kanuni hizi za ushirika, urafiki, na utambulisho zimeweka msingi wa dhana mpya ya umoja halisi wa kiekumene, aina ambayo inaweza kusababisha ushirikiano wenye upeo mkubwa na kiini chenye kina. Ufuatao ni muhtasari mfupi wa msingi wa kibiblia wa TUMI wa aina ya ushirikiano ambao unaweza kuchochea na kudumisha harakati za kuaminika za kupanda makanisa miongoni mwa maskini wa mijini. 1 Kor. 3:1-9 - Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. 2Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, 3 kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? 4 Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? 5 Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. 6 Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. 7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. 8Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. 9 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. Washirika na Watenda Kazi Pamoja na Mungu Ili Kuwezesha Harakati Anzilishi za Upandaji Makanisa Miongoni mwa Jamii za C 1 Ambazo Hazijafikiwa Kama huduma ya World Impact, TUMI imejizatiti kuzalisha na kuwezesha kimkakati harakati za Kupanda Makanisa ya C 1 ya kienyeji yanayokusudiwa kufikia Dirisha la 80% la miji ya Marekani. Ili kufikia lengo hili, tutasaidia kuunda ushirikiano wa kimkakati

Made with FlippingBook Digital Publishing Software