Theolojia Katika Picha

/ 6 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Ili Tuwe Umoja (muendelezo)

kati na baina ya wamishenari na wachungaji wa mijini, wanatheolojia na wana-umisheni, makanisa na madhehebu, na watu binafsi na mashirika yenye nia ya Ufalme ili kuanzisha vuguvugu thabiti la upandaji makanisa ambalo litazidisha maelfu ya makanisa ya kiinjili ya C 1 yanayofaa kiutamaduni miongoni mwa watu maskini wa miji ya Marekani. Tutatoa utaalam wetu ili kuhakikisha kwamba makanisa haya kwa kila njia yanamtukuza Mungu Baba katika utambulisho wake wenye msingi wa Kristo, ibada na maisha ya jumuiya chini ya uongozi wa Roho, Fundisho la kihistoria, na utendaji na utume uliojengwa juu ya misingi ya Ufalme. I. Ushirikiano 1 Unahusisha Kutambua Umoja wetu wa Msingi katika Kristo: Tunashiriki Vinasaba Vile Vile vya Kiroho. A. Imani yetu katika Yesu imetufanya kuwa kitu kimoja. 1. 1 Yohana 1:3 – hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 2. Yohana 17:11 – Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. B. Umoja wa kimfumo kati ya Baba na Mwana, na watu wa Mungu , Yohana 17:21-22 – Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. C. Umoja wetu unatuelekeza katika jitihada za pamoja za kumtukuza Mungu Baba wa Bwana wetu , Rum. 15:5-6 – Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; 6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. D. Mapenzi ya Mungu kwa Mwili ni umoja katika nia na shauri , 1 Kor. 1:10 – Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software