Theolojia Katika Picha
6 8 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Ili Tuwe Umoja (muendelezo)
E. Ubatizo wa Roho Mtakatifu umetufanya kuwa mwili mmoja katika roho , 1 Kor. 12:12 13 – Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. F. Kiini hasa cha imani ya Biblia ni umoja , Efe. 4:4-6 – Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. G. Kifungo chetu cha ushirika kinazuia umoja na wale ambao hawajaunganishwa na Kristo , 2 Kor. 6:14-16 – Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. II. Ushirikiano 2 Unahusisha Kufadhiliana kwa Rasilimali Fedha, Watu, na Nyinginezo ili Kufadhili Kusudi la Pamoja: Tunashiriki Chanzo Kimoja, Meza Moja na Chungu Kimoja. A. Ushirikiano kati ya wale wanaotangaza Neno na kulipokea unahusisha baraka na utoaji halisi. 1. Mwanafunzi kumshirikisha mwalimu , Gal. 6:6 – Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. 2. Hili limeonyeshwa katika uhusiano wa Myahudi na Myunani katika Mwili , Rum. 15:27 – Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili. B. Nguvu ya umoja inaenea kwa wale ambao wameteuliwa na Mungu kuwatumikia watu wake , Kum. 12:19 – Jilinde nafsi yako usimwache Mlawi siku zote uishizo katika nchi yako.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software