Theolojia Katika Picha
/ 6 9
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Ili Tuwe Umoja (muendelezo)
C. Wale wanaofanya kazi wanastahili kutendewa kwa ukarimu na wale wanaofaidika na kazi hiyo . 1. Maneno ya Kristo kwa wanafunzi , Mt. 10:10 – wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake. 2. Imenukuliwa kutokana na Maandiko na mifano ya Agano la Kale , 1 Kor. 9:9 14 – Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng’ombe? 10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake. 11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. 13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili. 3. Heshima maradufu: heshima na kushirikishana rasilimali , 1 Tim. 5:17-18 – Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. D. Uhusiano wa Wafilipi na Paulo ni mfano wa aina hii ya ushirikiano muhimu . 1. Tangu mwanzo walishirikiana na Paulo kwa vitendo , Flp. 1:3-5 – Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, 4 sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha, 5 kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi. 2. Epafrodito alikuwa mjumbe wao aliyepeleka misaada yao kwa Paulo , Flp. 2:25 – Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software