Theolojia Katika Picha

7 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Ili Tuwe Umoja (muendelezo)

3. Wafilipi walishiriki kikamilifu katika kusaidia huduma ya Paulo tangu mwanzo , Flp. 4:15-18 – Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. 16 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. 17 Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. 18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu. III. Ushirikiano 3 Unahusisha Kushirikiana Pamoja kama Watenda Kazi Wenza na Washirika Wenza Katika Kazi ya Kuendeleza Ufalme: Tunalo Kusudi Moja na Kazi Moja. A. Ushirikiano unahusisha kila mtu na kila kusanyiko kuleta mezani uzoefu wao wa kipekee, mtazamo, na karama kwa ajili ya matumizi ya wote , Gal. 2:6-8 – Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; 7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa; 8 (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa). B. Ushirikiano wa kweli unahusisha kutambua uongozi wa Bwana, fursa, na baraka anazotoa kwa wale walioitwa kuwakilisha maslahi yake katika maeneo ambayo amewaongoza , Gal. 2:9-10 – tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; 10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya. C. Ushirikiano katika suala la kufanya kazi pamoja na kushirikiana pamoja unahusisha maono ya pamoja na kujitolea kwa jambo moja , kwa mfano, Timotheo, Flp. 2:19 24 – Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20 Maana sina mtu mwingine

Made with FlippingBook Digital Publishing Software