Theolojia Katika Picha
/ 7 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Ili Tuwe Umoja (muendelezo)
mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 21 Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 22 Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. 23 Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata. 24 Nami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibu. D. Maneno ya kipekee aliyoyatumia Paulo kuhusiana na washirika wake katika Injili 1. Mtenda kazi mwenza ( synergos ), Rum. 16:3, 7, 9, 21; 2 Kor. 8:23; Fil. 2:25; 4:3; Kol. 4:7, 10, 11, 14; Flm. 1, 24. 2. Mfungwa mwenza ( synaichmalotos ), Kol. 4:10; Flm. 23
3. Mtumwa mwenza ( syndoulos ), Kol. 1:7, 4:7 4. Askari mwenza ( systratiotes ) Flp. 2:25; Flm. 2 5. Mshirika mwenza katika kazi ( synatheleo ), Flp. 4:2-3
E. Orodha fupi ya washirika wa Paulo katika huduma (hawa waliambatana naye katika kila awamu na juhudi za kazi, watu wenye historia zinazotofautiana, karama, kazi, na wajibu mbalimbali katika njia ya huduma yake). 1. Yohana Marko (Kol. 4:10; Flm. 24)
2. Aristarko ( Kol. 4:10; Flm. 24 ) 3. Androniko na Yunia (Rum. 16:7) 4. Filemoni (Flm. 1) 5. Epafrodito (sawa na Epafra) ( Kol. 1:7; Flm. 23; Flp. 2:25 )
6. Klementi ( Flp. 4:3 ) 7. Urbano (Rum. 16:9) 8. Yesu (Yusto) (Kol. 4:11) 9. Dema (ambaye baadaye alirudi nyuma akaiacha imani), (Kol. 4:14; Flm. 24; 2 Tim. 4:20) 10. Tikiko (Kol. 4:7; Flp. 4:3)
Made with FlippingBook Digital Publishing Software