Theolojia Katika Picha

7 2 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Ili Tuwe Umoja (muendelezo)

11. Arkipo (Flm. 2) 12. Euodia ( Flp. 4:2-3 ) 13. Sintike ( Flp. 4:2-3 ) 14. Tertio (Warumi 16:22) 15. Fibi (Rum. 16:1)

16. Erasto ( Rum. 16:23 ) 17. Kwarto ( Rum. 16:23 ) 18. Trifena ( Rum. 16:12 ) 19. Trifosa ( Rum. 16:12 ) 20. Persisi ( Rum. 16:12 ) 21. Mariamu ( Rum. 16:6 ) 22. Onesiforo ( 2 Tim. 1:16-18 )

IV. Matokeo ya Kanuni za Ushirikiano katika Mwanga wa Maono ya TUMI Ili Kuwezesha Harakati Anzilishi za Upandaji Makanisa Miongoni mwa Jamii za C 1 Ambazo Hazijafikiwa Kama huduma ya World Impact, TUMI imejizatiti kuzalisha na kuwezesha kimkakati harakati za Kupanda Makanisa ya C 1 ya kienyeji yanayokusudiwa kufikia Dirisha la 80% la miji ya Marekani. Ili kufikia lengo hili, tutasaidia kuunda ushirikiano wa kimkakati kati na baina ya wamishenari na wachungaji wa mijini, wanatheolojia na wana-umisheni, makanisa na madhehebu, na watu binafsi na mashirika yenye nia ya Ufalme ili kuanzisha vuguvugu thabiti la upandaji makanisa ambalo litazidisha maelfu ya makanisa ya kiinjili ya C 1 yanayofaa kiutamaduni miongoni mwa watu maskini wa miji ya Marekani. Tutatoa utaalam wetu ili kuhakikisha kwamba makanisa haya kwa kila njia yanamtukuza Mungu Baba katika utambulisho wake wenye msingi wa Kristo, ibada na maisha ya jumuiya chini ya uongozi wa Roho, Fundisho la kihistoria, na utendaji na utume uliojengwa juu ya misingi ya Ufalme.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software