Theolojia Katika Picha
7 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Imani Ya Nikea
Twamwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Mwuumba wa mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Twamwamini Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana Pekee wa Mungu. Amezaliwa na Baba kabla ya zamani zote; yu Mungu kutoka katika Mungu, Yu nuru kutoka katika Nuru, Yu Mungu kweli kutoka katika Mungu kweli; Mzaliwa ambaye hakuumbwa; Mwenye uungu mmoja na Baba; kwa yeye huyu vitu vyote viliumbwa. Aliyeshuka kutoka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na kwa wokovu wetu, alifanyika mwili kwa uweza wa Roho mtakatifu katika Bikira Mariamu, akawa mwanadamu; Akasulubiwa kwa ajili yetu zamani za Pontio Pilato; aliteswa, akazikwa. Siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo maandiko Matakatifu:- Akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Baba; naye atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Na ufalme wake hauna mwisho. Twamwamini Roho Mtakatifu, Bwana mtoa uzima, atokaye katika Baba na Mwana, anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, aliyenenwa kwa vinywa vya manabii.
Tunaamini Kanisa moja, takatifu, la Kikristo la ulimwengu wote na la kimitume.
Tunatambua ubatizo mmoja wa ondoleo la dhambi. Twatazamia kufufuliwa kwa wafu na uzima wa ulimwengu ujao. Amina.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software