Theolojia Katika Picha

7 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Jinsi ya KUPANDA Kanisa Don L. Davis

Marko 16:15-18 - Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Fanya Uinjilisti

I. Fanya Maandalizi

Luka 24:46-49 - Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. 48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. 49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu

mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu. A. Unda timu ya kupanda kanisa. B. Omba. C. Chagua eneo na jamii lengwa. D. Fanya utafiti wa demografia na ethnografia.

II. Anza Kazi

Wagalatia 2:7-10 - bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa; 8 (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa); 9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; 10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya. A. Andikisha watenda kazi wa kujitolea na uwape mafunzo. B. Endesha matukio ya Injili (mikutano, n.k) na uinjilisti wa nyumba kwa nyumba.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software