Theolojia Katika Picha
/ 9 3
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)
III. Tunaisikiaje Sauti ya Mungu ?
A. Fahamu kile ambacho Mungu Roho amekwisha kukisema tayari: Neno la Mungu lililoandikwa
1. Maandiko ni kumbukumbu ya mwongozo wa Roho. Maandiko sio tu kipimo kisicho na makosa cha usahihi wa maelekezo ya kiroho au unabii, yenyewe pia ni mafunzo yetu katika kuitambua sauti ya Mungu.
2. Yohana 5:46-47 –Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini Mimi; kwa sababu Yeye aliandika habari zangu 47 Lakini msipoyaamini Maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?
B. Elekeza moyo wako kutii
1. Kwa kawaida, tatizo HALIKO katika kusikia kwetu!
a. Zab. 119:10 –Kwa moyo wangu wote nimekutafuta; usiniache nipotee mbali na maagizo yako!
b. Swali la msingi linalohusiana na maongozi ya Roho si kama nitaweza kumsikia Mungu akisema bali kama ninakusudia kutii anachosema.
2. Mungu ni kiongozi mwenye uwezo, anayezungumza kwa uwazi.
a. Yohana 10:2-5, 27 – Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa,
Made with FlippingBook Digital Publishing Software