Theolojia Katika Picha
9 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)
bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni…. 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
b. Mifano ya Maandiko inamwelezea Mungu ambaye watu watamsikia! (1) Lugha za picha zinazotolewa na Mungu kueleza uongozi wake zinasaidia sana. Mungu ni mfalme, mzazi, mchungaji. Swali la «Tunasikiaje?» ni hadimu sana katika Biblia. Yesu anasema kwa ujasiri kabisa kwamba kondoo wake wanaijua sauti yake. Kama wafalme au wazazi au wachungaji wote, Mungu hashindwi kuwasiliana nasi kwa njia ambazo tutaelewa. (2) Je, ni wangapi kati yetu, kwa mfano, wameona Shirika la TRA likipata ugumu wa kuwasiliana nasi tukuambia tunapaswa kulipa kodi? Je! ni wangapi kati yetu ambao husahau au hujisahaulisha tu tarehe ya kulipa kodi na wasiifikirie tena mara tu inapokuwa imepita? (3) Ni wangapi kati yetu ambao mkiwa watoto mlijikuta mahala fulani mkiwa na huzuni kubwa kwa sababu hamkuwa na uhakika kama mtaweza kutambua sauti za wazazi wenu. Ulifanya nini ukiwa mtoto mchanga ili kuhakikisha unapata uwezo wa kuwasikia na kuwaelewa wazazi wako? (4) Vivyo hivyo, Mungu huchukua hatua ya kwanza kuwajulisha watu wake mapenzi yake. c. Mungu anaponyamaza mara nyingi inamaanisha kwamba anatupa uhuru wa kuchagua chochote kati ya machaguo mengi mazuri ambayo ametuwekea, au vinginevyo, Mungu akinyamaza maana yake ni kwamba tunafanya kazi chini ya amri na maelekezo ambayo tayari alikwisha kuyatoa hapo awali [yaani hatuhitaji maelekezo mapya]. (1) Ikiwa Mungu anataka tufanye jambo fulani, atalifanya jambo hilo liwe wazi kwa kila moyo unaosikiliza. (2) Wakati Mungu tayari ametufunuliamapenzi yake kupitiaMaandiko, swali halitakuwa tena kwa habari ya tutasikiaje bali ni suala la utii.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software