Theolojia Katika Picha
/ 9 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)
d. Umuhimu wa moyo unaosikiliza. Kanuni ya msingi: Hatuwezi kuwa tunampuuza Mungu au kukwepa
kutii na kisha kudai kwamba Mungu hasemi chochote. (1) Kanisa la Mungu kama mazingira ya asili ya kusikiliza.
(a) M fano wa familia ni wa kweli. Watoto wangu walikuja nyumbani baada ya shule kila siku, walikula mezani pangu, waliishi nyumbani kwangu, na kushiriki katika maisha ya familia yetu. Kwa sababu walifanya hivyo, walikuwa na uhakika kwamba walisikia nilichotaka kutoka kwao. Ni lazima tufanye vivyo hivyo katika mwendo wetu wa kiroho. (b) T ukipuuza uhusiano wetu na familia ya Mungu na tusipotumia muda wetu mbele zake, na kusikia Neno lake, atasema, lakini uwezekano mkubwa ni kwamba hatutasikia sauti yake. Kwa upande mwingine, kushiriki kwa bidii katika maisha ya familia ni sehemu muhimu katika kujinga uwezo wetu wa kusikia na kusikiliza. (c) Katika uzoefu wangu mwenyewe Mungu mara nyingi huzungumza nami kanisani. Wakati mwingine kupitia mahubiri na wakati mwingine kupitia kitu kingine tofauti kabisa na mahubiri au msisitizo wa ibada. Jambo la msingi ni kwamba niko kwenye meza ya familia yake. Anaweza kuongea kupitia mhubiri au anaweza tu kunasa usikivu wangu na kuzungumza moja kwa moja na moyo wangu lakini lazima nishiriki katika familia ili kuwa na matarajio ya kupokea maongozi yake. Ikiwa tunakimbia mbali na hatuwi na wakati na familia ya Mungu (kama mwana mpotevu) hatuwezi, basi, kuwa na visingizio kwamba hatumsikii akisema chochote. (d) Kusikia sauti ya Mungu si lazima liwe jambo la faragha. Kunatokea katika jumuiya. Tunasikia sauti ya Mungu vizuri zaidi tunaposikiliza pamoja na wengine. (e) Wachungaji wetu na viongozi wetu wa kiroho wana nafasi ya kipekee katika mchakato huu.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software