Theolojia Katika Picha
9 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)
(f) Ebr. 13:17–Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi. (g) Kuzungumza na viongozi na wachungaji wetu ili kupata maarifa na ushauri wao ni hatua ya asili ya kuanzia katika suala zima la maamuzi pale ambapo mapenzi ya Mungu hayako wazi. (h) N dugu na dada zetu katika Kristo pia ni vyanzo muhimu vya kutujulisha nia ya Kristo kwetu. (i) 1 Kor. 12:7–Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. (j) 1 Kor. 14:26–Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. (k) Mit. 27:17–Chuma hunoa chuma, ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. (l) Mit. 11:14–Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. (m) Kuisikiliza sauti ya Roho ina maana kwamba lazima tusikilize ushauri wa jumuiya ya kanisa na viongozi wake. (2) Umuhimu wa usikivu. Ninalifanya kuwa ni jukumu langu kudumu katika uwepo wake Mtakatifu, ambamo ninajiweka kwa uangalifu na heshima kwa Mungu, ambamo naweza kuita UWEPO HALISI wa Mungu; au, kwa lugha nzuri zaidi, mazungumzo ya kawaida, ya kimya na ya siri ya nafsi yangu na Mungu, ambayo mara nyingi hunisababishia shangwe na kunyakuliwa kwa ndani, na wakati mwingine pia kwa nje, kwa ukubwa sana, kiasi kwamba ninalazimika kutumia mbinu fulani kuzidhibiti na kuzizuia kuonekana kwa wengine. ~ Ndugu Lawrence alinukuu kutoka kwa Dallas Willard. Hearing God .
Made with FlippingBook Digital Publishing Software