Theolojia Katika Picha

/ 9 9

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo Don L. Davis

Utangulizi: Ulimwengu tunaoishi sio ule unaoonekana kuwa halisi, lakini kwa kawaida ni ule ambao sisi au wengine wameutunga ili tuishi ndani yake.

Kuita ‘Kitu Kitu’

Waamuzi watatu kwenye kongamano la waamuzi wakijigamba kila mmoja kwa mwenzake kuhusu umahiri wao kama waamuzi wa ligi kuu: I. M wamuzi wa Kwanza: Wengine huiita mipira na wengine huiita shuti, lakini mimi huiita jinsi ninavyoona! II. M wamuzi wa Pili: Wengine huiita mipira na wengine huita shuti, lakini mimi huiita jinsi yalivyo! III. M wamuzi wa Tatu: Wengine huita mipira na wengine huita shuti, lakini si kitu hadi niite kitu! Ni nini kiini cha safari ya imani ya Ukristo, asili ya theolojia na mafundisho ya Kikristo, moyo wa maadili ya Kikristo, kiini cha tumaini la Kikristo? Ni Yesu Kristo. Yeye ndiye kiini cha chimbuko la imani na maisha ya Mkristo. Vili tulivyo, yote tunayoamini, na yote tunayoelewa kwamba Mungu anafanya ulimwenguni yanahusiana na mtu huyu wa kipekee, ambaye pamoja na upekee wake bado mnyenyekevu: • Ambaye tuna simulizi chache tu za kuzaliwa na hadithi kuhusu ujana wake • Ambaye hatuambiwi chochote kuhusu miaka ya maisha yake kuanzia umri wa miaka kumi na mbili hadi thelathini, hata na wale waliomwabudu zaidi. • Ambaye alihudumu kwa miaka mitatu tu, na kukataliwa na wenzake, watu wa nchi yake, na taasisi za kidini • Ambaye alikufa kwa aibu, aliuawa hadharani kati ya wezi wawili, na kuwekwa kwenye kaburi la kuazimwa. • Ambaye twafahamu kidogo sana kuhusu sura na utu wake • Ambaye hakusafiri maili 200 kutoka mahali alipozaliwa

Made with FlippingBook Digital Publishing Software