Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 0 1

U O N G O F U & W I T O

Neno Linaloita

S O M O L A 4

ukurasa 199  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utaweza kuelewa, kuelezea, na kutetea ukweli kwamba: • Neno linalotuongoza vyema kwenye wokovu na uongofu pia linatuita kuishi kama wanafunzi wa Yesu, tukiyatii mapenzi yake. • Neno hili linalotuita katika uanafunzi linatudai kwamba tujitoe kwa Yesu ili tuweze kumpenda zaidi, zaidi ya upendo mwingine wowote, ikiwa ni pamoja na ndoa na familia, kwa njia ambayo tunaweza kumtumikia yeye kama Bwana juu ya vyote. • Wito huo pia unatutaka kukumbatia utambulisho wetu mpya katika Kristo kama wageni na wasafiri katika ulimwengu huu, wanaume na wanawake wanaotenda na kufanya kazi kama raia wa Ufalme wa Mungu katikati ya ulimwengu, kama wawakilishi wa Yesu. • Tunaakisi maisha ya ufuasi pale tunapoitikia vyema wito wa kuishi kama watumishi wa kujidhabihu kwa utukufu wake. Kama watumwa wa Kristo, tunatoa wakfu vyote tulivyo na vyote tulivyo navyo ili kumtukuza na kutimiza mapenzi yake ulimwenguni, kama apendavyo Yeye. • Tumeitwa pia kuishi na kufanya kazi katika jumuiya, kama washirika wa familia tukufu ya Mungu katikati ya watu wa Mungu ( laos ). • Mwanafunzi wa Yesu ameitwa kuishi katika uhuru wa Yesu Kristo, kutumia uhuru wake kama fursa ya kutimiza Amri Kuu, na kutoa ushahidi wa wazi kwa kusudi la kuwaokoa wengine kwa faida ya Kristo. • Neno linaloita katika ufuasi, jumuiya, na uhuru pia linatuita kwenye utume. Kama mawakala wa Ufalme wa Mungu, tumeitwa kutimiza Agizo Kuu, kupigana vita na adui yetu wa kiroho Ibilisi, na kuakisi maisha ya Ufalme kupitia upendo na matendo yetu mema.

Malengo ya Somo

4

Made with FlippingBook flipbook maker