Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 0 2 /
U O N G O F U & W I T O
Njia Tunayoiendea
Ibada
Soma Mathayo 4:17-22. Kusudi lako katika maisha ni lipi? Mzigo wako mkuu katika maisha ni nini? Sababu yako kuu ni ipi, ambayo ni msingi wa vyote ulivyo navyo na yote ufanyayo, na ambayo pia inaamua «nani» unahusiana na kushirikiana nao, na «vipi» unaenenda na kutenda mambo katika maisha yako? Hakuna mtu anayeweza kuishi maisha yenye utajiri kikamilifu, au kufikia aina yoyote ya ufahamu wa kile anachopaswa kufanya pasipo kwanza kujua kile ambacho ameitiwa, na kile ambachoMungu anakitaka kimahususi na kibinafsi katika maisha yake. Os Guiness, katika kitabu chake cha kuvutia cha “The Call” (yaani, Wito), anazungumza juu ya shauku hii kubwa katika moyo wa kila mtu ya kufikia mahali pa kugundua kusudi lake kuu maishani. «Ndani ya mioyo yetu, sote tunataka kugundua na kutimiza kusudi la maisha ambalo ni kubwa kuliko sisi wenyewe. Kusudi kubwa kama hilo pekee ndilo linaloweza kutupatia msukumo wenye nguvu ili kufikia vilele ambavyo tunajua hatuwezi kuvifikia kwa nguvu zetu wenyewe. Kwa kila mmoja wetu kusudi halisi ni la kibinafsi na lenye shauku kubwa: kujua tuko hapa kufanya nini na kwa nini. Kierkegaard aliandika hivi katika Jarida lake: ‘Jambo muhimu ni kujielewa mwenyewe, kuona kile ambacho Mungu anataka nifanye; jambo kubwa ni kutafuta ukweli ambao ni kweli kwangu , kupata wazo ambalo kwa ajili ya hilo naweza kuishi na hata kufa ’” (Os Guinness, The Call. [Nashville: World Publishing, 1998, uk.3]). Yesu alikuwa akihubiri kwamba ufalme wa Mungu umekuja duniani, akiwaita watu waume kwa wake kuishi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu ambao umekuja katika Yeye. Alipokutana na Simoni na Andrea, na Yakobo na Yohana, jozi mbili za ndugu ambao uvuvi wa samaki ulikuwa wito na kazi yao, Bwana wetu aliwaita kwenye kusudi la juu, la kweli, na kuu zaidi ya yote. Kumfuata Yesu kama Bwana, kuitikia kwa utii Neno lake ambalo linaokoa na kufundisha – hili ndilo kusudi la maisha. Yesu alikuja kwa watu hawa, akawashirikisha tu wito wake wa kumfuata, na ahadi yake kwamba angewafanya wavuvi wa watu. Hakubadilisha tu kazi yao, alibadilisha maisha yao, na kuwaweka kwenye njia ya kuiendea ambayo ilizaa safari ya maisha isiyo ya kawaida, uongofu, mateso, na ushuhuda. Walisikia tu Neno lake mwenyewe na kuitikia kwa imani na utii. Neno hilo lililowaita kwenye imani liliwaita kwenye ufuasi, na kupitia Neno hilo, waligundua maana na kusudi la maisha yenyewe: kuleta utukufu na sifa kwa Mungu pekee kupitia utumishi kwa Mwanawe, Yesu Kristo. Bila kujali njia tunayosafiri leo, tukisikiliza kwa umaniki tutasikia mwangwi wa maneno yale ya Mwalimu wetu ukiendelea mbele, hata katika vichochoro na mitaa ya jiji yenye giza kuu. Yesu yu hai, na kwa Roho wake Mtakatifu anawaita wanaume na wanawake kwake ili waishi kama watumishi wake, wakumbatie mfumo huo wa maisha ya kusisimua na yasiyo ya kawaida, na kuruhusu Roho wake kufanya
ukurasa 199 2
4
Made with FlippingBook flipbook maker