Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 0 3
U O N G O F U & W I T O
upya maisha yao wanapomtii siku baada ya siku. Wanafunzi wa zamani (kama wanafunzi wote wa kweli wanavyofanya) waliitikia mara moja kwa Mungu kwa utiifu wa haraka, shauku ya kweli, na hamu ya kweli. Ingawa walikuwa na familia, majukumu, wajibu, na kazi, waliweka kila kitu chini ili kumfuata Yeye ambaye peke yake angeweza kuwapa kile ambacho wasingekipata ndani ya kitu kingine chochote: uzima wa milele. Katikati ya safari zako, kazini kwako, maishani mwako, je, umesikia na kuitikia wito wa Mungu katika Yesu Kristo? Je, ‘umeacha yote mara moja, na kumfuata’ kama walivyofanya ndugu hao wawili? Ukisikiliza, utamsikia akikupa Neno lile lile kuu la amri alilowapa. Ahadi yake ni hakika: “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” Hutaishi tena kwa ajili yako mwenyewe, bali utaishi kwa ajili ya utukufu wake, na kuwa shahidi kwa wengine wa wokovu wake mkuu na wa utukufu. Liitikie Neno lake, uwe mfuasi wake, toa utii wa haraka kwa Neno lake ambalo linakuita kwake, ili uwe mwanafunzi wake. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunakuomba kwamba Mwanao, Bwana aliye Hai, atamke neno ambalo litatuita kwako, neno linalotuita tuwe watu wako na kututegemeza kwa nguvu za Roho wako. Tumeitwa kwenye ufuasi, kwenye utumishi katika jumuiya, kwenye uhuru, na kwa ajili ya utume. Ruhusu Neno lako takatifu na la milele lisikike katikati yetu, na utupe ujasiri na shauku ya kulifuata Neno hilo kwa mioyo yetu yote, kukutumikia kwa furaha, kudumu katika mapenzi ya Mungu, kuufurahisha moyo wako na kukuletea wewe utukufu katika Kanisa. Asante kwa Neno linalotuita kwako. Katika Jina la Yesu, Amina. Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi, kwa kuwa umetuhuisha kupitia zawadi yako ya mbinguni. Tunaomba kwamba kwa rehema zako tupate imani thabiti kwako na upendo wa dhati sisi kwa sisi, kwa Yesu Kristo Mwanao na Bwana wetu. Amina. ~ Martin Luther. Devotions and Prayers of Martin Luther . Trans. Andrew Kosten. Grand Rapids: Baker Book House, 1965. uk. 39.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
ukurasa 199 3
4
Made with FlippingBook flipbook maker