Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 0 4 /
U O N G O F U & W I T O
Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 3, Neno Linalogeuza .
Jaribio
Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Warumi 10:8-13.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
Mkristo Anaweza Kupata Pesa Kiasi Gani?
Katika mojawapo ya vikundi vidogo vya uanafunzi vya wanaume katika kanisa, mjadala mkali umekuwa ukiendelea tangu walipoanza kujifunza Injili ya Luka. Luka 14:33 inasema, “Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Ndugu mmoja alifasiri andiko hili (pamoja na maandiko mengine ya Biblia) kusema kwamba haiwezekani kwa Mkristo kuwa tajiri, hata kuwa na vitu vyake binafsi, kwa kuwa andiko linasema kwamba ni lazima atoe mali zake zote. Ndugu wengine katika darasa hilo wanasema kwamba tafsiri ya namna hii inavuka mipaka ya ukweli halisi; wazo la kweli ni kwamba wanapaswa kuwa na utayari wa kuacha mali zao zote, na si kuziacha kabisa. Ni aina gani ya ufuasi inayojitokeza katika mazungumzo haya? Wazee wa kanisa hukutana kila Ijumaa jioni, muda ambao wengi wa wanaume na wanawake wanaweza kuhudhuria. Ndugu mmoja mpendwa aliazimia kwamba angehitaji kuondoka kwenye baraza la wazee kwa sababu Ijumaa jioni kwa miaka kadhaa iliyopita umekuwa usiku wake wa miadi ya kutoka na mke wake. Kwa kuwa Mungu angemtaka adumishe kipaumbele cha ndoa kwanza kabla ya kile cha kanisa, anadai kwamba hawezi tena kutumika katika Baraza la Wazee wa kanisa. Wajumbe wengine wa baraza hilo wanasisitiza kwamba, kwa maana moja, Kanisa na mambo yake kama kusanyiko la Mungu linapaswa kuchukua kipaumbele juu ya masuala ya ndoa na familia. Mzee huyo alisimamia Maandiko mengine ambayo yanaonekana kuelekeza kwamba familia lazima ichukuliwe kama kielelezo cha Kristo na Kanisa. Ni upande wa nani wa hoja unakushawishi zaidi hapa? Miadi na Mwenzi au Miadi na Huduma ?
1
ukurasa 200 4
4
2
Made with FlippingBook flipbook maker