Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 0 5

U O N G O F U & W I T O

Waalike kwenye Uanafunzi, Sio kwenye Wokovu

Kusanyiko la Wabaptisti lililo katika mtaa wa jirani tu linakumbwa na mkanganyiko kuhusu huduma zake za ibada. Mchungaji mpya, Mkristo mzuri na mwalimu makini wa Biblia, anaamini kwamba hakuwezi kuwa na wokovu wa kweli mahali ambapo hakuna dalili za kujitoa kikamilifu katika suala la uanafunzi. Kanisa hilo, mwishoni mwa ibada zake, lina kawaida ya kuwaalika wale waliohudhuria ambao hawajampokea Kristo waje kwake kwa imani na utii. Tangu mchungaji huyu mpya amefika, amehubiri sana kwamba ukikataa kumkiri Yesu kuwa Bwana wako basi huwezi kumpokea kama Mwokozi. Unampokea Yesu kama Mwokozi na Bwana, yote kwa pamoja, na sio moja kwanza na jingine baadaye. Hii inaonekana kwenda kinyume na yale ambayo baadhi ya mashemasi wameelewa juu ya “wokovu kwa neema kwa njia ya imani,” na mipaka ya kuufanya wokovu kuwa kazi ya Mkristo mpya badala ya zawadi ya Mungu. Tunapaswa kuuelewa jinsi gani mwaliko wa kumjia Kristo – unamaanisha nini?

3

Neno Linaloita Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

4

Sehemu hii ya kwanza inaangazia dhana ya Neno la Mungu kama Neno linaloita kwenye ufuasi. Mungu hatuleti tu kwa Kristo, anatuita tuziishi ajabu za Hadithi yake katika maisha ya kujitoa ya ufuasi. Neno lile lile linalotuita kwenye wokovu kwa njia ya imani linatuita tujitoe kwa Yesu bila masharti ili tuweze kumpenda sana, kuliko ndoa na familia, kwa namna ambayo tunaweza kumtumikia bila masharti. Tunapaswa kukumbatia utambulisho wetu mpya katika Kristo, na wito huu wa ufuasi unatudai sisi kuchukua utambulisho wa wageni na wasafiri katika ulimwengu huu, kama wale wanaotafuta kumheshimu Mungu na kuutafuta mji mpya wa Mungu katika utukufu. Wito wa ufuasi pia unajumuisha amri ya Mungu kwetu kuwa watumishi wa kujidhabihu kwa utukufu wake. Kama watumwa wake katika ulimwengu huu, vile tulivyo na vyote tulivyo navyo katika maisha haya vinapaswa kutolewa wakfu katika kumjua Mungu na kumfanya ajulikane. Lengo letu la sehemu hii ya kwanza ya Neno Linaloita ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno linalotuongoza vyema kwenye wokovu na uongofu pia linatuita kuishi kama wanafunzi wa Yesu, tukiyatii mapenzi yake.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook flipbook maker