Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 0 6 /
U O N G O F U & W I T O
• Neno hili linalotuita katika uanafunzi linatudai kwamba tujitoe kwa Yesu ili tuweze kumpenda zaidi, zaidi ya upendo mwingine wowote, ikiwa ni pamoja na ndoa na familia, kwa njia ambayo tunaweza kumtumikia yeye kama Bwana juu ya vyote. • Wito huo pia unatutaka kukumbatia utambulisho wetu mpya katika Kristo kama wageni na wasafiri katika ulimwengu huu, wanaume na wanawake wanaotenda na kufanya kazi kama raia wa Ufalme wa Mungu katikati ya ulimwengu, kama wawakilishi wa Yesu. • Tunaakisi maisha ya ufuasi pale tunapoitikia vyema wito wa kuishi kama watumishi wa kujidhabihu kwa utukufu wake. Kama watumwa wa Kristo, tunatoa wakfu vyote tulivyo na vyote tulivyo navyo ili kumtukuza na kutimiza mapenzi yake ulimwenguni, kama apendavyo Yeye.
I. Kama Wanafunzi wa Yesu Mwenyewe, Tumeitwa kwenye Uanafunzi. Kipengele cha Kwanza cha Wito Huu ni Agizo la Mungu Kwetu la Upendo Mkuu kwa Yesu Kristo.
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
A. Upendo huu mkuu kwa Yesu Kristo lazima uzidi upendo wetu kwa ndoa na familia.
ukurasa 200 5
4
1. Upendo kwa Kristo lazima uzidi upendo kwa ndugu na wazazi, Mt. 10.34-37.
2. Upendo kwa Kristo lazima pia uzidi upendo kwa mwenzi na watoto.
a. Mathayo 10:37
b. Luka 14:26
B. Upendo wetu kwa Kristo lazima uzidi ushirika wetu na ulimwengu na anasa zake.
Made with FlippingBook flipbook maker