Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 2 9

U O N G O F U & W I T O

utoe majibu mafupi kwa maswali ya msingi yenye lengo la kuhusianisha somo na huduma na maisha. Pia, wakati wa mtihani, ni muhimu ujiandae kwa maswali ya kunukuu au kuandika mistari ya kukariri ya kozi hii. Utakapomaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na uhakikishe anapata nakala ya mtihani wako. Tafadhali zingatia: Ufaulu wako katika moduli hii hauwezi kupimwa na kujulikana kama hautafanya mtihani wa mwisho na kukusanya kazi zote na kuzikabidhi kwa mkufunzi wako (Fomu ya Ripoti ya Usomaji, kazi ya kihuduma, kazi ya ufafanuzi wa Maandiko, na mtihani wa mwisho). Katika dunia yote, hakuna kitu chenye uwezo na nguvu kama Neno la Mungu linalogeuza na kuita, Neno kuhusu wokovu wa Mungu kwetu katika Yesu Kristo. Neno la Mungu ni chombo cha Mungu cha kumwandaa mwanamume au mwanamke wa Mungu kwa ajili ya huduma yake, na ikiwa utatumiwa kwa nguvu na Mungu, lazima uchukue kwa uzito wajibu wako wa kuwa mwanafunzi wa Maandiko Matakatifu. Mungu akupe neema ya kutoa moyo wako na nafsi yako kikamilifu katika kulisimamia Neno la Mungu, ili wewe mwenyewe, pamoja na wale wanaokusikiliza, nyote mpate kuhisi nguvu yake ya kuumba, kuhakikisha, kubadilisha na kuita. Acha Neno lake na liwe neno la mwisho kwetu katika moduli hii:

Neno la Mwisho kuhusu Moduli hii

4

Mithali 2:1-9

Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; 2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; 3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; 4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; 5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu. 6 Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; 7 Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; 8 Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. 9 Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema.

Made with FlippingBook flipbook maker