Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 2 8 /
U O N G O F U & W I T O
Sasa, mwishoni mwa somo hili, utawajibika kutumia maarifa ya kozi hii katika shughuli mahususi ya huduma ambayo mshauri wako ameidhinisha. Ili kuelewa kwa kweli umuhimu wa uwezo wa Neno katika kuokoa, kubadilisha na kuita, ni lazima tulitumie Neno kivitendo katika muktadha wa huduma. Ni lazima ulishirikishe katika hali ambayo wengine wanaweza kupewa fursa ya kupokea maarifa ambayo umeyapata katika kipindi cha kujifunza kwako. Masomo mengi ya kujifunza kupitia mafundisho haya yako wazi: Hebu fikiria, kwa muda, juu ya njia zote za vitendo ambazo mafundisho haya yanaweza kuathiri maisha yako ya ibada, maombi yako, mwitikio wako kwa kanisa lako, mtazamo wako kazini, n.k. La muhimu ni kwamba unatafuta kuhusianisha mafundisho haya na maisha yako, kazi, na huduma. Kazi ya huduma kwa vitendo imekusudiwa kwa ajili hii, na katika siku zinazofuata utakuwa na fursa ya kushirikisha maarifa haya katika muktadha halisi wa maisha na mazingira halisi ya huduma. Omba kwamba Mungu akupe kutambua njia zake unaposhirikisha wengine maarifa yako kupitia kazi yako ya huduma. Somo hili la mwisho juu ya ufuasi, jumuiya, uhuru, na utume limejaa maana nyingi kwa maisha na huduma yako. Je, umehisi au kugundua masuala yoyote, hali, au fursa zinazohitaji kueleweka kupitia kanuni ulizojifunza katika somo hili? Ni watu gani hasa ambao Mungu ameweka moyoni mwako ambao wanahitaji dua na maombi mahususi kwa kuzingatia somo hili? Chukua muda wa kutafakari hili, na upokee msaada unaohitajika kupitia ushauri na maombi kwa ajili ya yale ambayo Roho amekuonyesha.
Kuhusianisha Somo na Huduma
Ushauri na Maombi
4
MAZOEZI
Hakuna andiko la kukariri.
Kukariri Maandiko
Hakuna kazi ya kukusanya.
Kazi ya Usomaji
Kufikia hatua hii unapaswa sasa kuainisha na kufikia maamuzi kuhusu mapendekezo ya kazi yako ya huduma kwa vitendo na ile ya ufafanuzi wa maandiko (eksejesia), na kuhakikisha yameidhinishwa na mkufunzi wako. Hakikisha unaweka mipango yako vizuri mapema ili usichelewe kukamilisha na kukabidhi kazi zako.
Kazi Nyingine
ukurasa 206 14
Mtihani wa mwisho utakuwa wa kufanyia nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka kwenye majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kutoka kwenye maelezo ya somo hili, na maswali ya insha ambayo yatakutaka
Taarifa Kuhusu Mtihani wa Mwisho
Made with FlippingBook flipbook maker