Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 2 7

U O N G O F U & W I T O

Achana na Hilo. Achana na Suala la Vigezo vya Ushirika!

Katika mjadala wa hivi majuzi miongoni mwa wazee wa kanisa kuhusu hali ya ushirika kanisani, baadhi ya wazee wamekuwa wakidai kukomeshwa kwa vigezo vikali vya ushirika. Wengi wa watu huja kwa sababu ya mafundisho thabiti ya Biblia, ibada ya kina, na mazingira bora ya kiroho ya kanisa. Ni takriban 20% tu ya wale wanaohudhuria ibada ndiyo huja kwenye mikutano ya kimkakati ya kanisa, jambo ambalo linafanya watu wengi kuonekana kutokuwa na uhusiano wowote na maisha ya kila siku ya kanisa husika. Wengine wanadai kwamba lazima kuwe na njia ambayo tunaweza kutofautisha wale ambao ni washirika katika kanisa letu na wale ambao si washirika, na vigezo vya ushirika ndio njia rahisi zaidi ya kufanya hivyo. Je, ungechukua msimamo gani kuhusu hili? Je, unaweza kuhusisha vipi hoja yako na wito wetu wa kuishi katika jumuiya? Neno linaloita hutuongoza kwa ufanisi kwenye wokovu na uongofu, pia linatuita sisi kuishi kama wanafunzi wa Yesu, watiifu kwa mapenzi yake. Linatuita kwa ajili ya ufuasi, likitutaka kwamba tumpende Yesu kuliko upendo mwingine wowote, kama Bwana juu ya yote. Linatuelekeza tukubali utambulisho wetu mpya katika Kristo kama wageni na wasafiri katika ulimwengu huu, wanaoishi na kumwakilisha Yesu kama raia wa Ufalme wa Mungu. Linatutaka tuishi kama watumishi wa kujidhabihu kwa utukufu wake, tumtukuze katika mambo yote kama Roho wake anavyoongoza. Neno hili pia linatuita kuishi na kufanya kazi katika jumuiya, kama washirika wa familia tukufu yaMungu katika watuwaMungu ( laos ). Kama washirika wa watu wake, tumeitwa kuishi katika uhuru wa Yesu Kristo, tukitimiza Amri Kuu na kuutumia uhuru huo kuwaokoa wengine kwa ajili ya Kristo. Hatimaye, Neno lile lile linaloita kwenye ufuasi, jumuiya, na uhuru pia linatuita kwenye utume. Kama mawakala wa Ufalme wa Mungu, tumeitwa kutimiza Agizo Kuu, kupigana vita na adui yetu wa kiroho Ibilisi, na kuakisi maisha ya Ufalme kupitia upendo na matendo yetu mema. Ikiwa una nia ya kujifunza zaidi nini maana ya kukutana na Neno la Mungu ambalo linatuita kwenye ufuasi, jumuiya, uhuru, na utume, unahitaji kuvipa usomaji na uchambuzi wa kina vitabu vifuatavyo: Phillips, Keith. The Making of a Disciple . Old Tappan, New Jersey: Revell, 1981. Scott, Waldron. Bring Forth Justice . Grand Rapids: Eerdmans, 1980. Snyder, Howard A. Kingdom, Church, and World: Biblical Themes for Today . Eugene, Oregon: Wipf and Stock Publishers, 1985.

4

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

4

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook flipbook maker