Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 2 6 /

U O N G O F U & W I T O

MIFANO

Katika Jina la Yesu, Toka!

Dada fulani mpendwa amekuwa akiwatazama walimu mbalimbali kwa bidii katika vipindi vya televisheni vya kidini kuhusu umuhimu na mchakato wa huduma za ukombozi. Akiwa amesadikishwa kabisa na mafundisho hayo, ameanza kuwafundisha wanawake katika darasa lake la Shule ya Jumapili kwamba matatizo mengi ambayo waamini hukabiliana nayo yanatokana na kupuuza kwao kutoa mapepo katika maisha yao. Ameanza kujikita katika huduma hii, akifundisha mbinu za kuyatoa; kuyatambua, kuyakemea, na kudai ushindi juu yao. Baadhi ya akina dada hawakubaliani na fundisho hili, wakisema kwamba hakuna mahali popote ambapo Mitume wanatuelekeza tujihusishe na aina hii ya shughuli. Ungeshughulikiaje hali hii?

1

ukurasa 206  13

Wote Wameitwa Kwenda

Katika kongamano la hivi majuzi la umisheni kanisani, mmoja wa wamishenari wageni alifundisha kwamba, kwa kuwa Mungu ameliita Kanisa kwenye umisheni, kila mtu anapaswa kuchukulia kwamba ameitwa kwenda. Ukiamua kubaki na kutokwenda kule ambako Yesu hajulikani, lazima utolee maelezo uamuzi wako, kwa sababu Agizo Kuu ni kwenda, na ni agizo kwa Kanisa zima. Je, unaamini kwamba waamini wote wameitwa kwenda, au ni baadhi tu wameitwa kwenda, na wengine wameitwa kuwategemeza wanaoenda?

2

4

Midundo ya Nguvu kwa ajili ya Yesu

Ili kufikia baadhi ya watoto wa magenge katika mtaa wao, kikundi cha vijana kimeanza kufadhili baadhi ya matukio ya tamasha la muziki wa kufoka, ili kuwavuta watoto hao kanisani. Kikundi cha vijana kimekubali kabisa maono haya, baada ya kupaka rangi upya chumba cha vijana na kuweka kazi kadhaa za sanaa ukutani, kutumia baadhi ya mapato yao yaliyokuwa yamewekwa akiba ili kupata vyombo vizuri vya muziki («vizuri» = vyenye sauti kubwa!), pamoja na vifaa vya kucheza muziki maarufu kama seti ya DJ, n.k. Walipokabiliwa na lawama kwamba wanafanya huduma za kuwafikia wengine kwa mbinu za kidunia, vijana hao walisema, “Tunatumia uhuru wetu kuwaokoa wengine, kama Paulo.” Una maoni gani kuhusu hoja yao? Je, wajivunie nini katika nafasi zao? Kwa upande mwingine, wajiadhari na nini?”

3

Made with FlippingBook flipbook maker