Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 2 5
U O N G O F U & W I T O
³ Neno linalotuita kwenye ufuasi, jumuiya, na uhuru pia linatuita kwenye utume. Kama mashahidi wa Yesu Kristo, tumeitwa kutimiza Agizo Kuu, kupigana vita na adui yetu wa kiroho Ibilisi, na kuakisi maisha ya Ufalme kupitia upendo na matendo yetu mema.
Sasa ni wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu wito wa Mungu kupitia Neno lake juu ya maisha yetu. Vipengele hivi tofauti vya ufuasi, jumuiya, uhuru, na utume vinadai tafakari na ufafanuzi wa kila mara, na ni muhimu kuelewa jinsi dhana hizi zinavyohusiana na wewe katika maisha yako na huduma. Pitia maudhui haya haraka, na uamue ni maswali gani mahususi uliyo nayo sasa kuhusu suala la wito wa Mungu. Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, inawezekana kudai kuwa na wokovu wa kweli wakati huo huo kumkana Yesu kama Bwana katika maisha ya mtu? Elezea jibu lako. * Ikiwa wito ni wa kuingi katika jumuiya ya Kikristo, tufanye nini wakati hatuwezi kupata kanisa ambalo Yesu Kristo anaabudiwa na kutukuzwa kwa njia tunayoamini anapaswa kuabudiwa? Vipi kuhusu kutumia kanda, mitaala, vitabu, na vifaa vingine vya kufundishia – je vinaweza kuchukua nafasi ya mahubiri na ushirika katika Kanisa? * Kuna maadui gani wa maisha ya huru katika Kristo? Je, si hatari kuhubiri uhuru katika Yesu katika jumuiya zetu mjini, hasa pale ambapo watu huhusisha uhuru na kufanya chochote wanachotaka kufanya? * Una maoni gani juu ya mafundisho mengi leo kuhusu “afya na mali” kama ishara ya baraka, kibali na uwepo wa Mungu? Je, yote yana makosa? Je, mafundisho juu ya wito wa Mungu wa ufuasi yanahusiana vipi na aina hii ya mafundisho? * Je, ni jambo la hakika kabisa kwamba kuishi sawa sawa na wito wa Mungu kutavutia mateso na manyanyaso? Kwa nini ushindi ambao Yesu alitushindia sio wa moja kwa moja, yaani, kwa nini kile ambacho Yesu alifanya msalabani hakikumaliza mapambano yote kwa niaba yetu hapa duniani?
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
4
Made with FlippingBook flipbook maker