Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 2 4 /

U O N G O F U & W I T O

9. Je, kushiriki katika matendo mema ya huduma kwa wanyonge na maskini kunatimizaje wito wa Mungu katika maisha yetu?

MUUNGANIKO

Somo hili linalenga katika upana na kina cha wito wa Mungu juu ya maisha ya mtu anayesikia na kuitikia Neno la Mungu. Neno linatuita kwenye ufuasi, jumuiya, uhuru, na kushiriki katika utume. Neno lile lile linalotoa maisha mapya pia linatuita katika maisha ya utii mkubwa kwa Yesu Kristo kama wafuasi wake, tukitimiza wajibu wetu kama mabalozi katika ulimwengu huu. ³ Neno linaloumba maisha mapya ndani yetu kwa njia ya imani pia linatuita kuishi kama wanafunzi wa Yesu Kristo wenye msimamo thabiti, tukimtumikia yeye na Ufalme wake, na kuwa watiifu kwa mapenzi yake. ³ Baba anawaita wote wanaoamini kujitoa kwa Yesu bila masharti ili waweze kumpenda zaidi, na wapate kuishi kwa ajili yake tu kama Bwana juu ya yote. ³ Tuna utambulisho mpya katika Kristo kama wageni na wasafiri katika ulimwengu huu. Tunapaswa kuishi kama mabalozi wa Kristo ulimwenguni, tukiishi kama raia wa Ufalme wa Mungu katikati ya ulimwengu mwovu, tukimwakilisha Yesu. ³ Sisi ni watumishi, watumwa wa Yesu Kristo, tunaishi kwa kujitoa kwa utukufu wake. Kama wafungwa wake mwenyewe, kama watumishi wake, tunapaswa kutoa wakfu kwa furaha vyote tulivyo na vyote tulivyo navyo na tunapaswa kumtukuza na kutimiza mapenzi yake ulimwenguni, sawa sawa na maelekezo yake. ³ Kama watu tulioitwa kwenye ufuasi wa mtu binafsi, tumeitwa pia kuishi na kufanya kazi katika jumuiya, kama washirika wa familia tukufu ya Mungu katika watu wa Mungu ( laos ). ³ Kupitia kuzaliwa upya na kufanywa wana, Roho Mtakatifu amesababisha mwamini mpya kushiriki nasaba (DNA) ya kiroho ya Mungu, na kupitia hilo, kuwa mshirika wa familia na ukoo wa Mungu mwenyewe. ³ Kama washirika wa kusanyiko la watu wa Mungu, tumeitwa kuishi katika uhuru wa Yesu Kristo, kutumia uhuru wetu, si kama kifuniko cha dhambi bali kama fursa ya kuwapenda wengine (hivyo kutimiza Amri Kuu), na kutoa ushuhuda wa wazi kwa kusudi la kuwaokoa wengine kwa ajili ya Kristo.

Muhtasari wa Dhana Muhimu

ukurasa 205  12

4

Made with FlippingBook flipbook maker