Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 2 3

U O N G O F U & W I T O

» Neno linalotuita kwenye ufuasi, jumuiya, na uhuru, pia linatuita kwenye utume. Tumeitwa kutimiza Agizo Kuu, kupigana vita na adui yetu wa kiroho Ibilisi, na kuakisi maisha ya Ufalme kupitia upendo na matendo yetu mema.

Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kupitia kile ulichojifunza katika sehemu ya pili ya video. Katika kuelewa asili ya Neno linaloita, tunapata mwangaza katika utajiri wa maana ya kuwa mtu wa Mungu, na kuwa sehemu ya watu wake waliochaguliwa. Tafadhali jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Nini maana ya maneno ya kibiblia «kuzaliwa upya» na «kuasiliwa,» na dhana hizi hutusaidiaje kuelewa asili ya wito wa Mungu wa kuishi katika jumuiya? 2. Je, Roho Mtakatifu, kama Roho wa kufanywa wana, hutusaidiaje sisi kuishi na kufanya kazi kama washirika wa familia ya watu wa Mungu? 3. Ni zipi baadhi ya maana ya kauli kwamba Neno linatuita kuingia katika jumuiya ya waaminio? Kwa kuzingatia haya, je, inawezekana kuishi maisha ya ufuasi na kushindwa kuwa mshirika wa kusanyiko lenye afya la waamini? Elezea jibu lako. 4. Je, ina maana gani kusema kwamba tumeitwa kuishi katika uhuru ndani ya Yesu Kristo? Mungu alituweka huru kwa njia gani hasa, yaani, ni nini hasa hasa kilichotuweka huru? 5. Je, ni mambo gani ambayo Mungu alituweka huru kutoka kwayo? Na, je, tumewekwa huru na Mungu kwa ajili ya kufanya mambo gani? 6. Ni vizuizi gani ambavyo Bwana ameweka kwa uhuru wetu, kwa maneno mengine, kuna mipaka gani (ikiwa ipo) ya uhuru huu tunaofurahia? Je, tumewekwa huru kwa makusudi gani katika Kristo? 7. Tumeitwa kwenye utume. Je, ni maagizo gani au kazi gani mahususi zinazohusishwa na wito wa Kanisa wa kushiriki katika utume wa Mungu? 8. Ikiwa Yesu tayari ameshinda vita dhidi ya shetani na wafuasi wake, je, tunaitwa kufanya nini hasa tunapopigana na adui katika ulimwengu huu?

Sehemu ya 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

ukurasa 205  11

4

Made with FlippingBook flipbook maker