Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 2 2 /

U O N G O F U & W I T O

2. Sisi ni watu wa milki ya pekee ya Kristo, ambao tuna bidii kwa ajili ya matendo mema, Tito 2:14.

3. Tunapaswa kutafuta kutenda haki miongoni mwa watu wote, hasa wale wa jamii ya imani, Gal. 6:9-10.

4. Tumeitwa kuonyesha uhalisia wa imani yetu kupitia matendo ya upendo ya huduma, hasa kwa maskini na wajane.

a. Imani isiyoambatana na matendo ni imani tupu na mfu (Yak 2:14-26).

b. Upendo wa Mungu haukai ndani ya moyo wa mtu ambaye anapuuza uhitaji wa kimwili wa ndugu yake Mkristo, 1 Yoh. 3:16-18.

4

c. Dini ya kweli mbele za Mungu ni kuwatunza wajane na yatima, na kujilinda na dunia pasipo mawaa (Yak 1:27).

d. Yale tunayowafanyia au tunayoshindwa kuwafanyia maskini, wageni, wenye njaa, wenye kiu, wagonjwa, wafungwa, na walio uchi, yatahesabiwa kama tuliyomtendea au tuliyoshindwa kumtendea Yesu Kristo, taz. Mt. 25:31-46.

Hitimisho

» Neno linalotuita kwenye ufuasi wa mtu binafsi pia linatuita kuishi na kufanya kazi katika jumuiya ya Kikristo, kama washirika wa familia yake tukufu, katika watu wa Mungu ( laos ). » Neno linatuita kuishi uhuru katika Kristo, kupendana na kutumikiana tunaposherehekea maisha mapya na kutumia uhuru wetu kuwapata wengine kwa ajili ya Kristo.

Made with FlippingBook flipbook maker