Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 2 1
U O N G O F U & W I T O
b. Yesu ametangaza kwamba adui yetu mkuu, Ibilisi, anatenda kazi kwa msingi wa uongo na udanganyifu (Yohana 8:44).
c. Neno la Mungu lina nguvu katika kubomoa uongo na mawazo ambayo yamejiinua kinyume na elimu ya Mungu, 2 Kor. 10:3-5.
3. Kushuhudia na kuishi hadithi ya Mungu katika Neno la Mungu hulisha na kuimarisha imani yetu, na hutuwezesha kutumia silaha zetu kwa ufanisi.
a. Kwa kujilinda, tunapinga uongo wa shetani kupitia Neno la Mungu, kupitia ngao ya imani ambayo huzima mishale yote yenye moto ya adui.
(1) Waefeso 6:16 (2) Warumi 10:17
4
b. Kwa kushambulia, tumeitwa kuendeleza Ufalme duniani kote. Tunapotangaza Neno la hadithi ya Mungu katika Yesu Kristo, tunaweza kumkatisha tamaa adui yetu wa kiroho na kuharibu shughuli zake kupitia Upanga wa Roho.
(1) Mathayo 16:18 (2) Waefeso 6:17 (3) 2 Timotheo 3:16-17
C. Mungu anatuita kwenye huduma ya huruma na haki, kudhihirisha utukufu wa Ufalme wa Kristo kupitia matendo mema na huduma.
1. Tuliumbwa tutende matendo mema, ambayo Mungu ametuitia, Efe. 2:10.
Made with FlippingBook flipbook maker