Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 2 0 /

U O N G O F U & W I T O

2. Tunaanzia katika “Yerusalemu” zetu wenyewe hadi “Yudea” zetu na “Samaria” zetu, na kisha twende mpaka “mwisho wa nchi,” Mdo 1:8.

3. Sisi ni mabalozi wa Yesu Kristo, 2 Kor. 5:18-21.

a. Kila mtu anapaswa kuwa tayari kumjibu yeyote anayeuliza sababu ya tumaini lililo ndani yetu, 1 Pet. 3:15.

b. Sisi sote tunapaswa kuandaliwa kushirikisha habari za Kristo katika mzunguko wa marafiki, familia, na watu tunaoshirikiana nao, tukiihudumia neema ya Mungu kwa wengine, 1 Pet. 4:10-11.

B. Kama washiriki katika jeshi la Mungu, Mungu anatuita tushiriki katika vita vya kiroho dhidi ya adui yetu mkuu, Ibilisi.

1. Tunahusika katika vita vya kiroho dhidi ya nguvu za kiroho zinazotafuta kuzuia kusudi la Ufalme wa Mungu ulimwenguni, Efe. 6:12-13.

4

2. Tumeitwa kufichua na kukanusha uongo na hadaa za adui.

a. Kusudi la Ibilisi ni kuzuia kazi ya Mungu ulimwenguni kupitia uharibifu ambao ameusababisha na madhara yake kwa uumbaji wa Mungu, hasa wanadamu, Yohana 10:10. (1) Hupofusha fikira za wale wasioamini, 2 Kor. 4:3-4 (2) Huwakandamiza wale walio wahanga na vibaraka wake kupitia mfumo wa ulimwengu wa uasi chini ya udhibiti wake, taz. Mt. 4:1-11. (3) Huwatesa watu wa Mungu kwa njia ya mashtaka, upinzani, na vizuizi, taz. Ufu. 12:10.

Made with FlippingBook flipbook maker