Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 1 9

U O N G O F U & W I T O

4. Si kwa jambo lolote linalomkwaza mwamini aliye na dhamiri dhaifu, 1 Kor. 8:13 - Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.

5. Ni kwa mambo yale tu ambayo yanatoa fursa ya kuwapenda ndugu na dada zetu katika Kristo, Gal. 5:13 - Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.

6. Kwa mambo yale tu yanayomtukuza Mungu, 1 Kor. 10:31 – Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

7. Si kwa kitu chochote kinachowaudhi Wayahudi, Wayunani au Kanisa la Mungu, 1 Kor. 10:32 – Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu.

4

8. Ni kwa mambo yale tu yanayochangia kuwaleta wengine kwa Kristo, 1 Kor. 10:33 – vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.

III. Neno la Mungu Linatuita – Watu Wake – Kushiriki Utume, Kufanya Wanafunzi wa Yesu Kristo kati ya Mataifa Yote, Kushiriki katika Vita vya Kiroho dhidi ya Ibilisi, na Kuakisi maisha ya Ufalme kwa Upendo na Matendo Yetu Mema.

ukurasa 204  10

A. Kama washiriki wa ukuhani wa ulimwengu wote, Mungu anatuita kutimiza Agizo Kuu.

1. Amri kwa Kanisa ni kwenda na kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi, Mt. 28:18-20.

Made with FlippingBook flipbook maker